MGOMBEA
urais wa CCM, Dk John Magufuli amewataka wananchi kumchagua ili awe rais
wa tano ajaye wa Tanzania huku akiahidi kushughulikia masuala
mbalimbali ya wananchi na hivyo kuliletea Taifa maendeleo kwa muda wote
atakaokuwepo madarakani.
Akizungumza
na wananchi wa mkoani Lindi katika muendelezo wa kampeni zake, Dk
Magufuli alisema akichaguliwa kushika nafasi hiyo, pamoja na mambo
mengine atakayoyafanya atatumia utajiri wa gesi uliopo katika mikoa ya
Kusini, kutoa ruzuku kwa vifaa vya ujenzi ili kushusha bei na
kuwawezesha wananchi kujenga nyumba bora.
Amesema
pia atatumia nafasi hiyo kutafuta namna bora ya kuwainua wakulima wa
korosho, tofauti na utaratibu wa sasa wa stakabadhi ghalani, alisema
umekuwa ukiwasababishia umasikini mkubwa wakulima wa zao hilo.
Akiwa
Nachingwea, Ruangwa, Mtama na Lindi Mjini, Dk. Magufuli alisema tofauti
na wapinzani wanaoahidi kuondoa nyumba za nyasi na tembe nchi nzima kwa
siku 100 watakazokaa Ikulu, jambo alilosema ni ndoto, Serikali yake
itakachofanya ni kushusha bei ya mabati, saruji, nondo, misumali na
vifaa vingine vya ujenzi ili wananchi wajenge nyumba bora.
Akielezea
ni vipi atawezesha hilo kufanikiwa, Dk Magufuli alisema atatumia
utajiri wa rasilimali za Taifa ikiwemo gesi inayopatikanakatika Mikoa ya
Kusini na Bagamoyo, Pwani ili kutoa ruzuku katika vifaa vya ujenzi.
Lakini,
pia kuongeza viwanda vya bidhaa hizo ili kushusha bei kwa kiwango cha
juu. Alisema dalili za kushuka kwa vifaa hivyo, zimeanza kuonekana baada
ya kujengwa kwa Kiwanda cha Saruji cha Dangote mkoani Mtwara,
ambachokinatumia nishati ya gesi kwa uzalishaji, kilichowezesha kushuka
kwa bei ya saruji kutoka Sh 16,000 hadi Sh 8,000 na kwamba bei hiyo
itashuka zaidi atakapokuwa rais.
Alisema
pia ataziba mianya yote ya rushwa serikalini ili makusanyo ya fedha
hizo yatumike kuboresha maisha ya Watanzania wakiwemo wa Kusini, huku
akisema ushahidi wa utendaji wake kwa watu wa Kusini ni ujenzi wa
barabara za lami kutoka Dar es Salaam kwenda Lindi na Mtwara na baadaye
Tunduru na Songea.
Ili
kumwezesha kuingia Ikulu, mgombea huyo aliwaomba wakaziwa Mkoa wa Lindi
kufika katika vituo vya kupiga kura mapema asubuhi ya Oktoba25, huku
akisema kutokana na vitisho na vurugu zilizopangwa ili kuwatishia
wananchi hasa wanawake wasipige kura, kutakuwa na polisi wa kutosha ili
kulinda amani.
Akizungumzia
soko la korosho, Dk Magufuli alisema akiingiaIkulu atabadili mfumo wa
ununuzi wa korosho ili kuwezesha wakulima wa zao hilo kwa mikoa ya
Kusini, kunufaika na kuboresha maisha yao na kuachana na mfumo wasasa
ambao unawafanya wakulima kukopwa fedha zao bila kulipwa na hivyo kuwa
masikini.
Post a Comment