Katibu
wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda leo amefanya makutano na
waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume,
ambapo ametumia nafasi hiyo kutangaza namba za simu za uchangiaji kwa
Watanzania kwa ajili ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Teddy amesema watanzania wanaweza kuichangia
Taifa Stars kiasi chochote cha fedha kuanzia shilingi mia moja (TZS 100)
kwenda namba 0654-888868 (Tigo Pesa) na 0789-530668 (Airtel
Money) ambazo zitatumika kwa ajili ya motisha kwa wachezaji,
uhamasishaji/masoko na maboresho ya kambi za ndani na nje ya nchi.
Aidha
Teddy amesema Kamati ya Taifa Stars inaandaa utaratibu kwa ajili ya
washabiki watakaotaka kusafiri kuelekea nchini Algeria katika mchezo wa
marudiano, waweze kuchangia gharama za usafiri ili waweze kwenda kuipa
sapoti Stars katika mchezo wa marudaiano Novemba 17, 2015.
“KamatI
inaendelea na mchakato wa kukamilisha suala la kambi ya Taifa Stars, na
mpaka sasa tunasubiri majibu kutoka katika vyama vya soka vya vya nchi
tunazotaka kuweka kambi ambazo ni Afrika Kusini, Dubai na Oman kabla ya
kutangaza rasmi kambi itakapokuwa” Alisema Teddy.
Kamati
inawaomba watanzania, wadau, washabiki na wapenzi wa mpira miguu nchini
kuichangia timu ya Taifa kupitia namba zilizotolewa na pia kujitokeza
kwa wingi kuujaza uwanja wa Taifa siku ya mchezo wa tarehe 14 Novemba,
2015
Post a Comment