OFISI Usambazaji na Ugavi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Eliud Njaila akiwaonyesha waandishi wa habari vizimba vya kupigia kura siku ya uchaguzi. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema wapiga kura waliopoteza kadi zao za kupigia kura hawataruhusiwa kupiga kura katika uchaguzi utakaofanyika nchini kote siku ya Jumapili.
Akizungumza
katika mkutano wa vyama vya siasa na NEC mjini Dodoma leo, Ofisa
Mwandamizi wa tume hiyo William Kitebi, amesema watu hao hawataruhusiwa
hata kama majina na taarifa zao zipo kwenye Daftari la Wapiga Kura
(BVR).
“Hakuna jinsi ya kuwasaidia watu waliopoteza kadi zao za kupigia kura ,”amesema Kitebi
Hata
hivyo, Kitebi amesema kutokana na kasoro zilizojitokeza kwenye BVR kuna
baadhi ya mambo NEC wameyawekea utaratibu ili watu waweze kupiga kura.
Amesema
watu ambao namba za kadi zinatofautiana na zile zilizopo kwenye BVR
lakini taarifa nyingine ni sahihi wataruhusiwa kupiga kura.
“Kuna wale ambao picha zao hazionekani kwenye daftari lakini kadi za kupiga kura wanazo, hawa wataruhusiwa kupiga kura,”amesema.
Kuhusu
wale wapiga kura walioathiriwa na mipaka ya utawala, Kitebi amesema
maamuzi ya tume kuwa watu hao watapiga kura kwenye kata walizopo.
“Kuna
maeneo kulikuwa na mabadiliko ya mipaka ya kiutawala baada ya zoezi la
uandikishaji kama Kishapu (Shinyanga) na Kaliuwa (Tabora), wao
wataruhusiwa kupiga kura kwenye maeneo yao mapya,”amesema.
Kwa
upande wa wapiga kura ambao wanakadi za kupigia kura lakini hawaonekani
kwenye BVR, Kitebi amesema hao wamewekewa utaratibu utakaowawezesha
kupiga kura.
“Kama
kule Mbarali (Mkoa wa Mbeya), kuna watu kama 6,000 ambao hawaonekani
katika daftari lakini wanakadi na fomu zao zimejazwa na kuwasilishwa
tume hawa wanaruhusiwa kupiga kura,”amesema.
Post a Comment