Mshambuliaji wa timu ya Simba, Hamisi Kiiza ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Septemba.
Kwa kuibuka mchezaji bora, Kiiza atazawadiwa sh. milioni moja kutoka kwa mdhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom.
Kiiza
ambaye ameisadia Simba kufanya vizuri kwenye mwezi huo, ikiwemo kufunga
mabao matatu (hat trick) kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar aliwashinda
washambuliaji wa timu za Stand United (Elias Maguli) na Yanga (Amisi
Tambwe).
Ndani ya mwezi Septemba ambapo zilichezwa raundi tano, Kiiza amefunga jumla ya mabao matano.
Post a Comment