‘Host’ wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria .
Na Imelda Mtema
‘HOST’ wa Kipindi cha Wanawake Live,
Joyce Kiria ameonekana kuwewesekea matokeo ya uchaguzi baada ya mumewe
aliyekuwa akigombea Ubunge Jimbo la Mwanga kushindwa. Baada ya matokeo
kutangazwa, Joyce alijikuta akiandika waraka mzito kwenye ukurasa wake
wa Facebook akieleza jinsi alivyoyapokea matokeo hayo kwa maumivu.
“Nimeumia sana mume wangu kukosa ubunge
lakini najiuliza kwa nini walikuwa wakimkatalia kuhesabu kura kwa mara
ya pili? Hivi vitu vinaumiza sana, vikitokea lazima upatwe na kiwewe,”
alisema Joyce.
GPL
Post a Comment