Watu
38 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi K isutu wakikabiliwa
na mashtaka manne likiwamo la kutoa vitisho vya shinikizo kwa msimamizi
atoe matokeo ya Ubunge ya Mbagala bila ya kufuata utaratibu na kuchoma
maboxi 11 ya kupigia kura na karatasi za kupigia kura zenye thamani ya
Sh 2.2 milioni.
Akisoma
hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Joseph Maugo
akishirikiana na Wakili wa Serikali, Genis Tesha walidai mbele ya
Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru kuwa Oktoba 27,2015 katika eneo la Mbagala
Majimatitu kwa nia ya uhalifu walifanya mkusanyiko na kuleta hisia ya
uvunjifu wa amani.
Alidai
kuwa washtakiwa hao walifanya kosa hilo kinyume na kifungu cha 74 na
75cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho
2002.
Katika
shtaka la pili, wanadaiwa kuwa Oktoba 27,2015 huko Mbagala Majimatitu,
kinyume na kifungu cha 79 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16
iliyofanyiwa marekebisho 2002 washtakiwa hao walikusanyika na kufanya
waliyodhamiria kuyafanya na kusababisha uvunjifu wa amani na kuleta hofu
katika jamii.
Maugo
katika shtaka la tatu, washtakiwa hao kwa pamoja kinyume na kifungu cha
326(1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa
marekebisho 2002 walichoma maboxi 11 ya kupigia kura na karatasi za
kupigia kura zenye thamani ya Sh 2.2 milioni mali ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi.
Wakili
huyo wa Serikali katika shtaka la nne alidai kuwa siku hiyo ya tukio
washtakiwa hao, walitoa vitisho na kumshinikiza msimamizi wa uchaguzi
atoe matokeo ya ubunge ya Mbagala bila ya kufuata utaratibu wa sheria.
Washtakiwa
hao wanadaiwa kufanya kosa hilo kinyume na kifungu 89B (1)(b) cha
sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002.
Baada
ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa wote walikana na upande wa
mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi bado haujakamilika.
Hakimu
Mchauru alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao
wanaaminika ambao kila mmoja atasaini bondi ya Sh 2 milioni hata hivyo
washtakiwa hao walipelekwa rumande baada ya kushindwa kukamilisha
masharti hayo.
Kesi imeahirishwa hadi Novemba 12, 2015 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.
Post a Comment