Mwenyikiti Mstaafu wa Chama cha Wananchi Cuf, Prof Ibrahim Lipumba amesema Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha amekiuka sheria kwa kusitisha utangazaji wa matokeo kwani inaweza kuleta mgogoro wa kisiasa.
Akizungumza
katika mahojiano na kituo cha Azam Tv, Prof Lipumba amesema mwenyekiti
wa ZEC alipaswa kuita majaji na wajumbe wa tume na kujadiliana na
kuwatangaza walioshinda na lisichukuliwe kisiasa.
“Huwezi kufuta matokeo ya urais Zanzibar halafu useme uchaguzi wa Tanzania ni halali,”amesema Lipumba
Amesema
katika katiba ya Zanzibar Ibara 28 (2) inasema rais atachia madaraka
yake baada ya kumaliza miaka mitano na kuongeza kuwa mwenyekiti wa ZEC
amedai kuwa kuhairishwa kwa matokeo ya urais kumesababishwa na kuwa na
wapigakura wengi zaidi katika vituo kuliko wale walioandikishwa.
“Suala hilo walipaswa waulizwe wasimamizi na mawakala na kulalamika siku ile ya uchaguzi,”.alisema Lipumba
Post a Comment