Mgombea
wa urais kupitia tiketi ya chama cha CHADEMA Edward LOwassa amesema
kuwa hatokubali matokeo ya uchaguzi wa urais yanayoendelea kutolewa na
tume ya uchaguzi nchini Tanzania NEC.
Amesema kuwa ana ushahidi wa kutosha kwamba kuna udanganyifu uliofanyika.
Wanadai kwamba kura zilizohesabiwa katika maeneo tofauti haziambatani na matokeo yaliotolewa.
Lowassa
ameongezea kwamba maeneo yote ambayo walipata ushindi yamecheleweshwa
huku kukamatwa kwa maajenti wa chama hicho akidai kuwa ni ishara za
kutaka kuiba kura.
Post a Comment