Mgombea
wa nafasi ya kiti cha urais kupitia tiketi ya Chadema anayeungwa mkono
na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, Edwrad Lowassa
ameahidi kuthibiti tatizo la mgao wa umeme ambao umekuwa changamoto
kubwa kwa wananchi.
Mgombea
huyo wa nafasi ya urais Edward Lowassa ametoa ahadi hiyo huku
akionekana dhahiri kuchukizwa na ahadi zisizotekelezeka za kutatua kero
hiyo ya umeme ambapo amesema serikali atakayoiunda itahakikisha
inadhibiti kikamilifu suala la mgao wa umeme.
Mgombea
huyo anayeungwa mkono na asilimia kubwa ya vijana ambao ni zaidi ya
asilimia 65 kwa mujibu wa tume ya uchaguzi, ametumia jukwaa hili la
mkutano wa hadhara hapa Same kutoa onyo kwa shirika la umeme nchini
Tanesco.
James
Mbatia mwenyekiti wa NCCR mageuzi amesema umasikini wa watanzania
unachochewa na uongozi mbovu wa CCM ambao umekuwa ukitumia rasilimali za
taifa kwa manufaa ya kundi dogo la watu wachache.
Katika
siku yake ya kwanza ya kampeni mkoani Kilimanjaro amehutubia mikutano
ya hadhara katika maeneo ya Hedaru, Ndungu, Same na Mwanga ambapo pia
alipata fursa ya kuweka shada la maua katika kaburi la muasisi wa CCM
Peter Kisumo mjini Usangi.
Post a Comment