Mtandao
wa Asasi za kiraia wa kuangalia chaguzi nchini Tanzania TACCEO leo
umeeleza kushtushwa kwake na mabadiliko yanayofanywa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ndani ya tume ya taifa ya uchaguzi NEC huku
wakisema kuwa mabadiliko hayo hayana ishara nzuri kwa watanzania
hususani kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania.
Akizungumza
na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam Kaimu mwenyekiti wa
TACCEO wakili IMELDA LULU URIO amesema kuwa mabadiliko yanayofanywa kwa
sasa ni makubwa sana kufanyika katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi
kwa chombo chenye dhamana ya kusimamia mchakato mzima wa uchaguzi na
kuhakikisha ushiriki wa wananchi katika kupiga kura.
Amesema
kuwa kwa siku ya hivi karibuni imeshughudiwa mabadikilo makubwa ya
baadhi ya watendaji na makamishna wa tume hiyo huku akitolea mfano
mabadiliko yaliyofanyika tarehe 25 mwezi wa 7 mwaka huu ambapo rais
KIKWETE alifanya mabadiliko kwa kumuondoa aliyekuwa mkurugenzi wa
uchaguzi ikiwa imesalia miezi mitatu kabla ya siku ya kupiga kura,huku
pia Mkurugenzi wa technologia ya habari na mawasiliano TEHAMA wa tume ya
uchaguzi DK SISTI CARIAH akiondolewa kwenye nafasi hiyo kukiwa
kumesalia mwezi mmoja kupiga kura.
Mabadiliko
mengine ambayo TACEO wameonyesha kuwa na wasiwasi ni kuteuliwa kwa
makamishna wawili wa tume hiyo zikiwa zimebaki siku 39 kabla ya siku ya
kupiga kura ambapo walioteuliwa kushika nafasi hiyo ni pamoja na Jaji
mstaafu wa mahakama kuu ya Tanzania,MARY LONGWAY na wakili ASINA A,OMARY
Wakili
IMELDA amesema kuwa mtandao huo unaitaka serikali kuhakikisha kuwa
hawafanyi mabadiliko ya tume ya uchaguzi kwa kuwaondoa watendaji wake
kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha mapungufu ya kiutendaji ndani
ya tume na kupelekea wananchi kukosa imani na tume hiyo.
Aidha
katika hatua nyingine mtandao huo wa TACCEO umeitaka tume ya taifa ya
uchaguzi NEC kuhakikisha kuwa inatangaza na kuweka wazi orodha ya vituo
vya kupigia kura mapema ikiwa ni pamoja na kuweka daftari la wapiga kura
siku 14 kabla ya uchaguzi ili wananchi waweze kuhakiki majina yao na
kufahamu vituo wanavyostahili kutumia kupiga kura.
Mtandao
wa kuangalia chaguzi nchini Tanzania TACCEO unaoratibiwa na kituo cha
sheria na haki za binadamu LHRC umekuwa ukishiriki katika uangalizi wa
mchakato wa uchaguzi nchini kuanzia zoezi la uandikishwaji wapiga kura
kwa kutumia mfumo mpya wa kielektonic BVR, mchakato wa kuwapata wagombea
ndani ya vyama,kampeni za Urais,wabunge na madiwani kuelekea mchakati
mzima wa uchaguzi wa tarehe 25 october mwaka 2015.
Post a Comment