Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mabasi yapigwa mawe kwa ushabiki wa kisiasa

Mabasi mawili ya Kampuni ya Zacharia Express mali ya Pita Zacharia mkazi wa Tarime mjini yanayofanya safari zake Tarime-­Mwanza yameharibiwa kwa kupondwa na mawe kwa kile kinachoelezwa ni ushabiki wa kisiasa. 

Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya Lazaro Mambosasa alisema kuwa Octoba 26, majira ya saa tisa mchana katika kijiji cha sokoni,Kata ya Sirari,Wilayani Tarime Gari lenye namba za usajili T.562 CAP aina ya YUTONG iliyokuwa ikiendeshwa na Joseph Magazin ikitokea katika kituo cha mabasi cha Sirari kuelekea katika egesho la kituo cha mafuta ilipigwa mawe. 

Mambosasa alisema gari hilo lilishambuliwa kwa kurushiwa mawe na kuvunjwa kioo cha mbele,vioo vine vya madirisha upande wa kulia na vioo vitatu vya madirisha upande wa kushoto vyote vikiwa na thamani ya 6,500,000. 

Aliongeza kuwa siku hiyo hiyo majira ya saa sita mchana gari lingine lenye namba za usajili T.925 CZM aina ya YUTONG iliyokuwa ikiendeshwa na Ezekia Merico(32) Dereva mkazi wa Isamilo Mwanza ilishambuliwa kwa mawe na kuvunjwa kioo kimoja cha Dirisha la nyuma upande wa kulia lenye thamani ya 2,000,000. 

Mambosasa alisema kuwa Magari hayo ni mali ya Kampuni ya Zakaria Express, na kwamba watuhumiwa wawili wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo ambao ni Libaya Msabi (34)mkazi wa Remagwe na Marwa Juma(17) mkazi wa Sokoni Sirari
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top