THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Ndugu Joel Laurent kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu
Tanzania (TEA). Uteuzi huo ulianza Oktoba 18, mwaka huu, 2015.
Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Laurent alikuwa Katibu wa Taasisi hiyo ya TEA na ndiye amekuwa anakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
26 Oktoba, 2015
Post a Comment