Magavana
wa Afrika wakutana na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa Bi.
Christine Lagarde na Rais wa Kundi la Benki ya Dunia Dr. Jim Yong Kim
kujadili namna ya kuchochea maendeleo na kuimarisha uchumi barani
Afrika.
Ujumbe
wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu
wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile wakisalimiana na Mkurugenzi wa
Shirika la Fedha la Kimataifa Bi. Christine Lagarde wakati akiingia
kwenye ukumbi wa mkutano.
Katikati
ni Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa Bi. Christine Lagarde
akinukuu hoja zilizokuwa zikijadiliwa katika mkutano huo.
Magavana
wa Afrika wakiwa kwenye Mkutano wa majadiliano na Mkurugenzi wa Shirika
la Fedha la Kimataifa Bi. Christine Lagarde na Rais wa Kundi la Benki
ya Dunia Dr. Jim Yong Kim nchini Peru – Lima.
Wa
pili kulia ni Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt.
Servacius Likwelile akifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mkutano.
Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi Benki Kuu ya
Tanzania Dr. Joseph Masawe.
Ujumbe wa Tanzania wakiwa kwenye mkutano wakujadili namna ya kuimarisha
uchumi na kuchoche maendeleo Barani Afrika. Kutoka kushoto ni Kamishna Idara ya
Sera Bw. Bedason Shallanda, Mhasibu Mkuu Msaidizi Bw. Ishmael Kasekwa, John
Mavura mchumi Wizara ya Fedha na Bw. Patrick Pima mchumi Wizara ya Fedha.
Imetolewa na
Msemaji wa Wizara ya Fedha
Bi. Ingiahedi Mduma
13/10/2015
Post a Comment