TAARIFA
Alipokuwa
akizungumza kwenye kongamano maalum huko Zanzibar, aliyekuwa
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mh Othman Massoud Othman alielezea wajibu
wa kila Mzanzabari wa kuutetea umoja wa Wazanzibar.
Akifafanua
kifungu cha 23 cha Katiba ya Zanzibar, Bw. Othman alielezea kuwa, mbali
na Katiba hiyo kutoa haki sawa kwa Wazanzibari wote, pia inatoa wajibu
kwa wananchi.Miongoni mwa wajibu wa kila Mzanzibari kwa mujibu wa
Kifungu hicho, ni wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha Uhuru wa
Zanzibar, Mamlaka ya Zanzibar, Ardhi ya Zanzibar na Umoja wa Zanzibar.
Maelezo
hayo ya Mheshimwia Othman, yanakwenda sambamba na malengo makuu ya
Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Marekani (ZADIA).Kwa hivyo, ZADIA
inapenda kuchukua fursa hii kumpongeza na kumuunga mkono Mheshimiwa
Othman Massoud Othman kwa kauli zake hizo za kizalendo alizozitoa
tarehe10/10/215 mjini Unguja.
Bwana
Othman alikumbusha jinsi alivyotekeleza wajibu wake huo wa kikatiba
kivitendo kwa kupiga kura "kama alivyopiga" kwenye Bunge Maalum la
Katiba kule Dodoma.Aidha, alifafanua kasoro zilizomo kwenye Katiba
pendekezwa ya Tanzania ambazo alizielezea kuwa hazina maslahi kwa
Zanzibar.
Kitendo
hicho cha kijasiri, na maelezo hayo, vinatoa changamoto kwa Kila
Mzanzibari kuiga mfano huo. Nasi Wanadiaspora tumezipokea kwa moyo wote
changamoto hizo na kuzifanyia kazi kama ambavyo imekuwa kawaida yetu.
Natutafanya juhudi zote na tutashirikiana na wadau wote, ili kuhakikisha
kuwa Zanzibar inapata hadhi yake na haki zake ndani ya Muungano wa
Tanzania.
Omar H. Ali,
Mwenyekiti,
Post a Comment