Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akihutubia wananchi baada ya
kupokea matembezi ya amani ya vyama vya siasa yaliyofanyika kuanzia eneo
la Magomeni hadi viwanja vya Kinondoni Biafra Dar es Salaam leo
asubuhi.
Mwenyekiti wa Wilaya ya Chama cha Union For Multi Party Democratic (UMD), Abdallah Tumbo akihutubia katika mkutano huo.
Katibu wa Wilaya ya Kinondoni wa Chama cha UDP, Makoye Ikoles, akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Wilaya wa Chama cha UPDD, Salim Choya akizungumza katika mkutano huo.
Katibu wa CCM wa Wilaya ya Kinondoni, Athuman Shesha akihutubia katika mkutano huo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Amani wa dini zote Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad
Mussa Salum, akiongoza dua za kuombea nchi amani katika mkutano huo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Amani wa dini zote Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad
Mussa Salum akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni katika mkutano
huo.
Dua la kuombea taifa ikiendelea.
Vijana wa Joging wakishiriki matembezi hayo.
Matembezi yakiendelea.
DC Makonda (katikati), akiwa na Viongozi wa vyama vya siasa walioshiriki maandamano hayo.
Vijana wa Jogging wakiwa jukwaa kuu wakiimba wimbo maalumu wa amani.
Na Dotto Mwaibale
Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda amesema kila mtu ana wajibu wa kuilinda
na kudumisha amani iliyodumishwa na waasisi wa nchi hii hasa katika
kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka
huu.
Makonda
alitoa mwito huo wakati akihutubia wananchi baada ya kupokea matembezi
ya kuombea nchi amani yaliyofanyika katika viwanja vya Biafra Dar es
Salaam leo.
Maandamano hayo yameratibiwa na Makonda katika wilaya yake kwa niaba ya watanzania wote.
Makonda
alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi chache zilizodumu kwa amani na
amani hiyo ilidumishwa na waasisi wa Taifa hivyo imebaki kuwa kimbilio
na tegemeo kwa watanzania.
Alisema
ili kuwaenzi waasisi hao ni kutunza tunu hiyo na kwamba yapo mataifa
yamepita katika nyakati mbalimbali za uchaguzi lakini hawana amani kama
tuliyonayo hivyo tuna wajibu mkubwa kuitunza.
"Vipo
viashiria vya uvunjifu wa amani, lakini ikumbukw kuwa amani ni kubwa
kuliko ahadi za mgombea yoyote wa chama cha siasa hivyo hakuna
kinachoweza kufanywa na mgombea yeyote kama hakuna amani,"alisema.
Hata
hivyo Makonda alisema kuwa aliandika barua kwa kila chama cha siasa
ambapo vyote vilithibitisha kushiriki lakini cha kushangaza baadhi
havijahudhuria kwa kutoa sababu zisizo na msingi wowote kama kutokuwa na
nauli na mambo mengine.
"Niliviandikia
barua vyama vyote, lakini vingine havijahudhuria kwa makusudi hivyo
dalili mnayoona hapa ni dalili tosha kuwa amani wanayohubiri kwenye
majukwaa si hii wanayoitaka,"alisema Makonda.
Makonda
aliongeza kuwa vyama vilivyoshiriki katika maandamano hayo ya amani ni
CCM, CUF, UPDP, UDP,UMD, Jahazi asilia na vilabu vya Jogging .
Akizungumza
katika mkutano huo Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es
Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum alisema mtu yeyote asiyependa amani ni
adui wa Mungu.
Sheikh
Alhad aliitoa kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam leo wakati alipoongoza
dua maalum ya kuombea amani wakati wa maandamano ya vyama vya siasa
yaliyofanyika kuanzia eneo la Magomeni hadi viwanja vya Kinondoni
Biafra.
Alisema
kuwa anavipongeza vyama vilivyothibitisha kushiriki maandamano hayo
pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Konondoni, Paul Makonda na kamati ya ulinzi
kwa kuandaa shughuli hiyo.
Alisema
kuwa kuna baadhi ya vyama ambavyo vilitakiwa kushiriki lakini
havijashiriki ambapo havijaathiri chochote na kuweka wazi kuwa wachache
wanaweza kufanya mambo kwa ajili ya wengi.
"Kuna
baadhi ya vyama havijashiriki maandamano haya, hivyo vikumbuke kuwa watu
wachache wanaweza kufanya mambo kwa ajili ya wengi hivyo ni jambo kubwa
na kwamba mungu analisikia,"alisema.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti baadhi ya viongozi na wawalikishi wa vyama hivyo
walisema kuwa watanzania wanapaswa kupiga kura kwa amani pia
walishamaliza wakatulie nyumbani kusubiri matokeo kutoka kwa mawakala
wanaowaamini waliowaweka vituoni.
Post a Comment