Mjane
wa aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
Dk. Emmanuel Makaidi, Modesta Ponela Makaidi akiwa katika huzuni baada
ya kuondokewa na mpendwa wake.
Mtoto wa kwanza wa Dk. Makaidi, Hilda Emmanuel Makaidi akizungumza na wanahabari (hawapo pichani)
Mtoto wa marehemu Mhandisi Emmanueli Makaidi (kulia), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ratiba ya mazishi ya baba yake.
Ndugu, jamaa, marafiki na waombolezaji wakiwa msibani nyumbani kwa Dk.Makaidi Sinza.
Mjane
wa aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
Dk. Emmanuel Makaidi, Modesta Ponela Makaidi (kulia), akiwa na
waombolezaji wengine nyumbani kwake Sinza Vertican Dar es Salaam kesho
asubuhi.
Na Dotto Mwaibale
MWILI
wa Mwenyekiti Mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) Dk. Emmanueli Makaidi unatarajiwa kuagwa kesho katika viwanja
vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, mtoto wa marehemu Mhandisi
Emmanueli Makaidi alisema mwili huo baada ya kutoka Masasi ulipelekwa
Hospitali ya Jeshi ya Lugalo na leo jioni utapelekwa nyumbani kwa
marehemu maeneo ya Sinza Vertican ambapo itafanyika ibada fupi na kupata
fursa ya ndugu na majirani kuuaga.
Alisema
kesho mwili huo utaagwa katika viwanja vya Karimjee ambapo viongozi
mbalimbali wa kisiasa, serikali watakuwepo na kisha kufanyika mazishi
yake katika makaburi ya Sinza.
"Unajua
baba alikuwa ni mwanasiasa na amefariki akiwa bado ni mwanasiasa hivyo
ni lazima uweze kuagwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na
serikali" alisema.
Akimzungumzia
baba yake alisema marehemu alikuwa ni mtu ambaye anapenda utu ambapo
alipenda kila binadamu ni sawa na hapaswi kubaguliwa.
Alisema
wameamaua kumzika baba yao Dar es Salaam na si Mtwara kutokana na mke
na mama yake kuzikwa Dar es Salaamna ndio utaratibu waliouweka wa
kuzikwa.
"Baba alitaka kila mtu ambaye atafariki ni vyema akazikiwa hapo kwani hata wakati wa kulimia makaburi inakuwa rahisi,"alisema.
Kwa upande wake mtoto wa pili wa Marehemu Hilda Makaidi alisema baba yao alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu.
"Nakumbuka
nilimpigia baba simu akiniambia mwanangu Hilda Masasi kugumu, na mimi
nikamwambia baba rudi nyumbani tukutibu lakini hakukubali
haraka,"alisema.
Alisema baba ameacha mjane na watoto 10 huku ikiwa wakike wakiwa wanne na wakiume sita na wajukuu 10 na vitukuu sita.
Kwa
upande wake Katibu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi George Kahangwa
alisema mazishi hayo yatahuduliwa na mgombea urais wa umoja huo Edward
Lowassa pamoja na viongozi wa taifa wa serikali na vyama vya siasa na
vyama vya michezo.
"Sote tushiriki kumpa heshima za mwisho na kumsindikiza mpendwa wetu katika safari ya mwisho,"alisema.
Post a Comment