Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema wamegundua njama za kuiba kura zitakazofanywa na CCM usiku wa tarehe 24 kwa kupita mitaani na kugawa fedha za kura feki.
Mbowe alitoa kauli hiyo jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe vilivyopo jijini Mbeya.
Alisema
ili kudhibiti hali hiyo, siku hiyo Ukawa watafanya doria usiku kucha
ili kuhakikisha hakuna fedha zinazogawiwa wala kura feki
zitakazosambazwa.
“Nia
ya Ukawa ya kupigania Katiba ya wananchi iko pale pale kwani Serikali
ya awamu ya tano itaipigania kadri itakavyowezekana ili kiu ya wananchi
juu ya Katiba hiyo ipatikane,” alisema Mbowe.
Alisema
pia kwamba, uchaguzi wa mwaka huu ni wa kihistoria kwa kuwa unahusu
maisha ya watu, watoto na utajibu maombi ya Watanzania.
Pamoja
na hayo, alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), siyo huru na kwamba
wanachama wa Chadema watahakikisha wanalinda kura zao.
“Kwa
miaka 25 tumepiga kelele tukidai tume huru ya uchaguzi lakini kilio
chetu hakikusikika kwa sababu CCM inajua tukiwa na tume huru, haiwezi
kubaki madarakani.
“Kama
tume yetu siyo huru, tuna wajibu wa ziada wa kulinda kura zetu. sheria
inasema huturuhusiwi kusimama wala kukaa chini ya mita 200 kutoka
kituoni. Kwa hiyo, ukihesabu mita 200 kutoka kituoni, una uhuru wa kuwa
eneo hilo,
“Jambo
hili limezua hofu ndani ya tume, ndani ya Serikali, ndani ya CCM na
kwa Rais Jakaya Kikwete kwa sababu anasema tukishapiga kura, tukalale.
Sasa namwambia Rais Kikwete ushauri huo akawape CCM, sisi hatuutaki,” alisema Mbowe.
Alisema
pia kwamba, wanachama wa Chadema na wapenzi wao, hawatafanya fujo bali
watakuwa na ujasiri wa kupiga na kulinda kura zao kwa sababu hakuna
anayeweza kuzuia mpango wa Mungu kwa kutumia askari au nguvu.
Post a Comment