Mkurugenzi wa taasisi ya Mkubwa na Wanawe, Said Fella 'Mkubwa Fella' akiwa na baadhi ya mtoto katika hospitali hiyo.
Mkurugenzi wa taasisi ya Mkubwa na Wanawe, Said Fella 'Mkubwa Fella' akikabidhi msaada katika hospitali ya Mbagala Zakhem Jijini Dar es Salaam ikipokelewa na Dk. Silas Adam.
Mwandishi Wetu
TAASISI
ya Mkubwa na Wanawe inayomilikiwa na Mkurugenzi wake Said Fella 'Mkubwa
Fella' jana ilitembelea Wodi ya Wanawake na Watoto katika Hospital ya
Mbagala Zakhem Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari Hospitalini hapo ambapo alikuja kutoa vifaa
mbalimbali kwa wagonjwa sambamba nakufanya usafi katika eneo la
hospitali hiyo.
Fella
alisema, ameguswa kuitembelea hospitali hiyo na ataendelea kufanya
hivyo kupitia umoja wa vikundi vya Joging saba alivyoviunda katika kata
yake ya Kilungule anakowania Udiwani.
"Tumekuja
hapa Hospitali kuwasalimia wagonjwa na tumewaletea kitu kidogo
tulichojaaliwa kama unavyoona Sabuni, dawa za meno, soda, juice na vitu
mbalimbali,"alisema Fella.
Akizungumzia
msaada huo Dk. Silas Adam alimshukuru Fella kwa sapoti yake na kuona
umuhimu wa kuwatembelea wanawake na watoto katika Hospitali hiyo.
Silas
alisema, licha ya shukurani hiyo ya vifaa hivyo amemuomba Fella
kuwasaidia damu kupitia vijana wake hao kwani wanachangamoto kubwa ya
damu hasa katika wodi ya wazazi.
"Tunamshukuru
sana Fella kwa kidogo alichojaliwa kukileta kwetu ni faraja kubwa sana
kwetu, tunatambua alivyotoa mchango mkubwa kwa vijana hapa nchini. hivyo
basi kupitia vijana wake hao tunakuomba utusaidie waje watoe
damu,"alisema.
Aliongeza
kwa kuwataka Watanzania wengine kuwa na moyo kama wa Fella kusaidia
watu mbalimbali hata kama sio katika hospitali hiyo.
Naye
Mwenyekiti wa umoja wa vikundi hivyo vya jogging Salimu Omary alisema
wametembelea hospitali hiyo ikiwa ni siku moja kabla ya kuzindua umoja
wao kupitia kata ya Kilungule ambapo uzinduzi huo unafayika leo.
mwisho
Post a Comment