Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe akihutubia wananchi wa Makete
Wananchi
wapenda mabadiliko wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kulinda
kura zao baada ya kupiga na kukaa umbali wa mita 200 toka kilipo kituo
walichopigia kura
Hayo
yamesemwa na mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA
Freeman Mbowe wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika
viwanja vya mabehewani Makete mjini jana ambapo pia aliambatana na
mgombea urais wa chama hicho Edward Lowassa
Mbowe
amesema haiwezekani kwa hali ilivyo sasa nchini wananchi wakapiga kura
na kwenda nyumbani kwa kuwa kumekuwa na viashiria vya kukosekana
uaminifu ambavyo vitasababisha wizi wa kura
"Wangapi
mtakubali kupiga kura na kwenda nyumbani? Mnataka nani awalindie kura
zenu? Mnataka muwaachie CCM wawalindie?, Sheria inasema hivi ukishapiga
kura nenda umbali wa mita 200 toka kilipo kituo, subiri matokeo yako
hapo, huo ndio utaratibu, iweje leo waseme tuende nyumbani baada ya
kupiga kura?" amesema Mbowe
Hivi
karibuni tume ya taifa ya Uchaguzi NEC imewataka wananchi kupiga kura
na kuondoka vituoni kuelekea majumbani kama njia mojawapo ya kuepusha
vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyoweza kujitokeza, jambo ambalo
limekuwa likipingwa na vyama mbalimbali vya siasa hasa vya upinzani
Post a Comment