Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia anaungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, hana uwezo wa kumfufua aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), marehemu Daud Balali.
Membe
ambaye jana alionekana kwa mara ya kwanza katika kampeni za mgombea
urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, alisema Balali alikufa kifo
cha kawaida na hataonekana tena.
Akizungumza
na wakazi wa Lindi Mjini kwenye kampeni za mgombea huyo wa urais wa
CCM, Membe alisema anajua vizuri namna Balali alivyougua hadi kufariki
dunia, hivyo mgombea kuahidi kumleta mtu aliyekufa ni jambo la
kushangaza.
Membe
alisema Balali aliugua maradhi ya utumbo na kwenda kutibiwa nchini
Marekani mwaka 2008 na baadaye alifariki dunia na kuzikwa kwenye
makaburi ya huko huko.
“Lowassa aache kujifanya Yesu kwamba atafufua wafu,” alisema...."nimesikia hata hapa Lindi ameshafika, sasa kamwambieni yeye si Yesu na wala hana uwezo wa kumfufua Balali,” alisema Membe.
Membe
alisema kama kweli Lowassa anaamini kwamba Balali amefichwa na
serikali, basi aende akamtafute alikofichwa na amlete na kumwonyesha
hadharani.
Aidha,
alisema Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, wamekuwa
wakidai kwamba serikali haijafanya lolote tangu uhuru wakati nao
walikuwa na nafasi kubwa serikalini.
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM, Salma Kikwete, naye aliibuka jana kwenye
kampeni za Dk. Magufuli kwa mara ya kwanza na kusisitiza kuwa Dk.
Magufuli ndiye chaguo bora.
Alisema rais mwenye uwezo wa kuwaletea maendeleo ya kweli na ya haraka, ni Dk. Magufuli.
Kwa
upande wake, mgombea ubunge Jimbo la Mtama, Nape Nnauye, alisema ingawa
kuna wanaomwandama, lakini tayari yeye ndiye atakuwa mbunge wa jimbo
hilo kwa miaka mitano ijayo.
Alisema
wananchi wa Lindi na Mtama wameshaamua kumpa kura zote Dk. Magufuli kwa
sababu wanaami kuwa rasilimali gesi na mafuta iliyogundulika mkoani
humo itakuwa salama.
Kwa
upande wake, Dk. Magufuli alisema anataka gesi iliyogunduliwa katika
mikoa ya Mtwara na Lindi iwanufaishe Watanzania wote wakiwamo wa mikoa
hiyo.
Alisema
atahakikisha makampuni ya nje yanayokuja kuwekeza kwenye mikoa hiyo
yanaajiri wakazi wa mikoa hiyo kwa nafasi mbalimbali badala ya kwenda na
watu wao.
Post a Comment