|
Taarifa zaidi kuhusu Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki na kujeruhiwa huko Saudi Arabia
Mahujaji
wengine wanane kutoka Tanzania ambao walikuwa hawaonekani tokea ajali
ya kukanyagana kwa mahujaji ilipotokea Makkah nchini Saudi Arabia tarehe
24 Septemba 2015 wametambuliwa kuwa, ni miongoni mwa mahujaji
waliofariki dunia.
Kutambuliwa
kwa mahujaji hao kunafanya idadi ya mahujaji wa Tanzania walipoteza
maisha katika ajali hiyo kufikia ishirini (20). Majina kamili ya
mahujaji hao na vikundi vilivyowasafirisha kwenda Makkah katika mabano
ni Hamida Llyas Ibrahim (Khidmat Islamiya), Farida Khamis Mahinda (Ahlu
Daawa), Archelaus Anatory Rutayulungwa (Khidmat Islamiya) na Said
Abdulhabib Ferej (Ahlu Daawa).
Wengine
ni Awadh Saleh Magram (Khidmat Islamiya), Salama Rajab Mwamba (Khidmat
Islamiya), Nuru Omar Karama (Ahlu Daawa) na Saida Awaadh Ali (Ahlu
Daawa).
Serikali
ya Saudi Arabia inaendelea kutoa taarifa zaidi za mahujaji waliofariki
dunia au kujeruhiwa katika ajali hiyo na Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu
wahanga wa ajali hiyo kadri itakapokuwa inazipokea.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
13 Oktoba, 2015
|
on Wednesday, October 14, 2015
Post a Comment