Kuhudhuria
kwenye mikutano ya kampeni za wagombea ni raha, maana kuna mambo mengi
hususan vioja, maneno matamu, vituko na vijembe vya wagombea.
Kwa mfano mgombea ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Sambwee Shitambala
(CCM), juzi alitoa kali mbele ya wananchi wa Kata ya Ruanda, aliposema
akichaguliwa hawezi kuvaa tena nguo za kijani kwa kuwa atakuwa ni mbunge
wa wananchi na siyo chama.
“Niwahakikishie tu wananchi, mchakato wa CCM ulishapita, hivyo
watakaonichagua ni wananchi wa Mbeya Mjini. Kwa hiyo mimi sitavaa sare
za CCM ofisini na kwenye mikutano yangu ili kutoa fursa sawa,” alisema
Shitambala.
Mbali na hilo, alimponda mmoja wa wagombea wenzake katika jimbo hilo
akidai ametengeneza kiwanda cha ‘machizi’ ambao kazi yao ni kuzomea tu
na kuleta vurugu na maandamano
Post a Comment