Butiama ni
mji uliopo kaskazini mwa Tanzania, katika wilaya ya Musoma mkoa wa
Mara. Mahala hapa ndipo alipozaliwa Rais wa Kwanza wa Jamuhuri wa
Muungano wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere(Baba wa
Taifa), ambapo leo ni siku ya kukumbuku ya kifo chake (13 April 1922-14
Octoba 1999)
Kijiji hiki
kina historia Kubwa ambapo leo imekuwa siku muhimu ya kukumbuka mahala
alipozaliwa shujaa wa Tanzania aliyepelekea uhuru na umoja wa nchi yetu.
Ndani ya kijiji cha Butiama
kuna vingi vya kujivunia na kufanya mji huu ukawa maarufu hasa ndani na
nje ya nchi, kuna miji mingi imekuwa maarufu kwa kupewa kipaumbele na
wazawa mfano; mahala alipozaliwa Mandela (Afrika kusini) ambapo kumekuwa
na watalii wengi wanaongezeka kila mwaka na watalii wengine hutokea
Tanzania. Basi tuwe na desturi hii pia ya utalii wa ndani katika kijiji
hiki cha Butiama kilicho ndani ya mji wetu.
Jovago
Tanzania inapendelea kuorodhesha baadhi ya vivutio katika mji huu
ambavyo ni muhimu iwapo utakuwa na hamu ya kuutembelea mkoa wa Mara
katika Kijiji cha Butiama.
Kaburi la Baba wa Taifa; Mbali na kuwa na kumbukumbu za mahala alipozaliwa, pia ndipo kaburi la baba wa Taifa linapopatikana
Hiyo ndiyo nyumba ambayo kaburi limo.
Uwepo wa Jumba la Makumbusho la Mwalimu Nyerere;
Hapa utaweza kujua historia nzima ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere, harakati zake za kisiasa na maisha halisi aliyoishi katika uhai
wake, vifaa vya nyumbani alivyotumia, na aina ya mavazi aliyopendelea
kuvaa.
Mwenge wa Mwitongo; Je unapafahamu mahala pa Mwenge wa Uhuru unapozimwa na kuwashwa kama ishara ya kumuenzi Mwalimu?
Kabila la Wazanaki; kihistoria inaaminika ni kabila lenye watu wachache kulinganisha na makabila mengine katika mji wa Musoma.
Kabila hili lipo katika kijji cha Butiama “Mwitongo” ikimaansha
“mahame” yaani ni eneo lililokuwa na wakazi ambao walihamia sehemu
nyingine. Eneo hili ni muhimu kuhistoria na utaweza kuifahamu iwapo
utafika hapa.
Hata hivyo
mkoa wa Mara unasehemu nyingi mbali na Butiama ambazo unaweza kutembela
na ukaona ufahari wa nchi yetu kihistoria na kijiografia. Uwepo wa Ziwa
Victoria kama kivutio cha watalii wengi, na hifadhi ya wanyama pori ya
Serengeti iliyopo katika wilaya ya Serengeti.
Usafiri na malazi; Mji
huu umeendelea hasa katika usafiri wa anga na nchi kavu, ni rahisi
kuchukua ndege zinazoelekea Mwanza kupitia Musoma, au mabasi ya mikoani
yanayoelekea Musoma, na Mara.
Pia, kuna hoteli nyingi zenye bei nafuu, JovagoTanzania
imeingia ubia na zaidi ya hoteli 21 katika ndani ya kijiji cha Butiama
ambapo inarahisisha mtu yeyote kubook (kujihifadhia) hoteli zenye ulinzi
na huduma za kutosha iwapo ataingia kwenye tovuti ya Jovago na kuchagua
hoteli atakayopendelea.
Imechotwa: Mo Blog
Post a Comment