Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikweteakimnadi mgombea wa urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano mkubwa wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Jangwani Dar es Salaam.
Wananchi wakishangilia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Jangwani jijini Dar es Salaam.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano mkubwa wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi uliofanyika kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu.
Hakuna
haikuwa rahisi kusogeza mguuu wala kusogea eneo moja kwenda jingine
kutokana na idadi ya watu waliofurika kumshuhudia Dk.Magufuli ambaye
anagombea urais huku Mwenyekiti wa ccm taifa Rais Jayaka Kikwete akisema
tayari mgombea wao ameshinda urais.
Mkutano
wa kumuombea kura Dk.Magufuli ulifanyika Dar es Salaam jana ambao sauti
za watu zilizosikika kwenye eneo hilo walisikika wakiimba Dk.Magufuli
rais na rais kikwete akieleza wazi Rais wa awamu ya tano ni Magufuli.
Kikwete amuita Magufuli Rais
Akizungunza
mbele ya maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam , Rais kikwete
alisema Rais wa awamu ya tano ni Dk.Magufuli na kuongeza sifa zake
huwezi kufananisha wagombea wa vyama vingine.
Rais
Kikwete alisema Rais ni Magufuli na wengine ni vivuli vya urais na
kuwahakikishia watanzania kuwa hana mashaka hata kidogo baada ya
uchaguzi mkuu kufanyika kesho kinachofuata ni kuapishwa kwa mgombea
urais wa CCM.
Alisema
Dk.Magufuli amezunguka nchi nzima kwa gari na kote alikopita
amehutubia wananchi zaidi ya saa moja na kueleza yale ambayo ametumwa
na chama wakati kuna mgombea ametumia helikopta lakini wameshindwa
kuhutubia.
Alisema
wakati Dk.Magufuli anazunguzia kila mahali na wananchi mgombea wa
Chadema anashindwa kueleza sera na kuwambia wananchi wakasome kwenye
web site (mitandaoni).
"
unawaambia watu wakasome kwenye website na watu wanajiuliza hiyo
website iko wapi.mgombea urais kwenye sifa ni Dk.Magufuli tu na hao
wengine ni vivuli vya urais. Dk.Magufuli anawapenda vijana na mgombea
pekee aliyezungumzia kupambana na rushwa.
*Mgombea
yule mwingine hana sifa ya kuzungumzia rushwa na ufisadi kwani hana
uwezo wa kupambana nayo.zaidi rushwa na ufisadi utastawi na kwa Magufuli
rushwa itadhibitiwa na ndio maana anaeleza kutoka moyoni namna ambavyo
atakabiliana nayo ikiwa pamoja na kuanzisha mahakama ya wazi.
Rais
Kikwete alisema Dk.Magufuli anakubalika kutokana na sifa mbalimbali
alizonazo ikiwemo ya uadilifu na utumishi uliotukuka na kuongeza Mgombea
urais wa CCM ametimia kwa sifa na anatosha kwa kila upande na huyo ndio
John Magufuli anayemjua yeye na ndio maana Ccm ilimchagua.
Alisema
Magufuli kwenye kipindi cha kampeni amezungumzia namna ambavyo ameweka
mipango ya kuongeza soko la ajira huku akijikita katika kueleza namna
ambavyo atasimamia haki kwa watu wote.
"Magufuli
ndio Rais sahihi wa awamu ya tano ,ameelezea makundi mengi
atakavyoyatumikia na kuongeza Magufuli amesema namna atakavyowezesha
wanawake kujishughulisha na uamendeleo yao na kuongeza kuwa ameahidi
kuongeza fedha kwenye benki ya wanawake.
"
Hivi kwa akina mama mna mtu Kama Magufuli mnahangaika na hao wengine
wanini? Wakazi gani? Mpeni kura Magufuli awatumikie.Mtu wa aina ya
Magufuli unamuachaje kumpa kura.
"Wenzetu
wale hata siku moja hawajahi kuzungumza namna ambavyo atasaidia kundi
la walemavu bali wao wanazungumzia kumtoa babu seya. kwa Magufuli
ameeleza namna ambavyo atasaidia kundi la walemavu," alisema.
Rais
Kikwete alisema Dk.Magufuli ameishi maisha ya watu masikini na anatoka
familia ya wakulima na wafugaji hivyo ni atashughulia maisha ambayo
ameyaishi.
Amchambua Kingunge
Rais
Kikwete alisema kuwa kuna ametoka CCM akidai utaratibu wa kumpata
mgombea urais wa CCM bali kilichotokea mzee huyo aliyemtaka hakupita.
Alisema
utaratibu uliofanyika mwaka 1995 ndio ambao umetumika mwaka huu wa 2015
na kuongeza mzee (Kingunge ngambare mwiru) alikuwa na mtu wake hakupita
na ndio sahihi anahaha kumtetea.
"Kuna
mzee anazunguka na kudai utaratibu umekosewa si kweli .Mwaka 1995
Kingunge alikuwepo wakati huo huo na kilichotokea utaratibu uliotumika
wakati ile ndio huo huo," alisema Rais Kikwete.
Alisema
kuwa hao ambao wapo upande wa pili wamekosa hoja na sasa wanahangaika
na hata wengine kuzungusha mikono wanashindwa huku akiomba watanzania
kumchagua Dk.Magufuli awe Rais wa awamu ya tano.
Azungumzia amani siku ya uchaguzi
Wakati
huo huo, Rais Kikwete alisema kuwa siku ya uchaguzi mkuu utakuwa wa
amani kwani serikali imejipanga vema na hakuna mahala ambapo kutatokea
vurugu.
Pia
alisema upinzani ulikuwa imekwend mahakamani kwa ajili ya kutaka wakae
mita 200 kwa kigezo cha kulinda kura na kilichotokea walikwenda
mahakamani na hatimaye wameshindwa.
Magufuli na urais
Kwa
upande wake mgombea urais wa CCM Dk.Magufuli alisema kuwa amezunguka
kwenye kampeni kwa gari ambapo ametembea zaidi ya kilometa 46000 na kote
huko wanasema Rais ni Magufuli hivyo anaamini baada ya jumapili Rais
atakuwa yeye.
Dk.Magufuli
alisema atakuwa Rais wa watanzania wote na ndio maana baada ya kuanza
ziara ya mkoa w Dar es Salaam alipokelewa na vyama vyote ikiwa pamoja na
kuweka bendera mpya Kama ishara ya yeye kuwa rais mpya wa awamu ya
tano.
Alisema
kuwa matarajio yake katika kuwatumikia watanzania katika kuwaletea
maendeleo na kuongeza yote ambayo anayasema kwenye kampeni anayaweza
kutekeleza.
Alisema
dhamira yake ni kuwa serikali ya viwanda ili kuinua uchumi wa
watanzania na kuongeza waliochukua viwanda na wameshindwa kuviendeleza
watanyang'wanywa ili wapewe wengine watakaoviendeleza.
Dk.Magufuli
alisema anafahamu mambo yanayohitajika kufanywa maeneo mengi ya nchi
yetu lakini kwa kuwa yupo Dar es salaam lazima azungumzie mambo
yanayohusu mji huo na kuongeza mji huo lazima changamoto za msongamano
umalizwe na kutatua shida ya maji.
Akizungumzia
barabara za Dar es Salaam ,Dk.Magufuli Alisema kwenye awamu yake kuna
barabara kadhaa ambazo zinatakiwa kujengwa kwa lami na kuongeza kuna
maeneo yanatakiwa kupandishwa hadhi ili serikali ipeleke huduma muhimu
kwa wananchi ambapo mabilioni ya fedha yatatumika.
Alisema
ili kuondoa au kupunguza msongamano serikali ya awamu ya tano ,
itajenga barabara za juu katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es
Salaam huku akieleza kutaanzishwa mfuko maalumu kwa ajili ya kuboresha
barabara za Jiji hilo.
Dk.Magufuli
alisema barabara ya juu eneo la Tazara itaanza kujengwa kwani tayari
mkandarasi amepatikana na ataanza kujenga huku huku akieleza kuwa kwake
amedhamiria kumaliza msongamano uliopo kwa mipango sahihi aliyonayo.
Pamoja
na yote hayo aliwaomba wananchi wa Dar es salaam kuwa wamchague awe
Rais ili afanye kazi huku madereva wa nchi yetu akiahidi kuboresha
maisha yao kwa kuangalia upya mikataba yao na wakati huo huo akieleza
namna ambavyo atafuta ushuru kwani ni kero.
Akitumia nafasi hiyo kuwa dhamira yake ni kuboresha maisha ya wanachi na hiyo kazi anaweiza ndio maana ameiomba.
"Mawazo
yangu ni kuboresha msongamano wa magari na nieleze tu nitaanzisha njia
barabara ambazo zitatumia waendesha bodaboda kwani nao wanahaki ya
kuongia mjini. naitwa tinga tinga sasa nipeni kura za kutosha nitinge
Ikulu," alisema Dk.Magufuli.
Aliwahakikishia
wakazi wa Dar es salaaam kuwa anakuwa karibu nao maana kwani ndio
amelelewa na wananchi wa mkoa huo na kuongeza urais utakuwa wake na
umati unaojitokeza kwenye mikutano yake inatosha kusema tu yeye ndio
rais wa awamu ya tano.
Watu wazimia
Wakati
huo huo eneo hilo la mkutano ambalo lilikuwa na idadi kubwa ya wananchi
wapi baadhi ya wananchi walizimia kwa kukosa hewa na hiyo ilisababisha
watoa huduma ya afya kuwa n jukumu la kutoka huduma.
Pia
polisi walikuwa na kazi ngumu ya kidhibiti idadi ya watu waliokuwa
wanataka kujinasua kwenye kundi la watu kwa kupita eneo ambalo lilikuwa
na uzio .
Hata
hivyo walilazimika kufungua sehemu ya uzio ili kupunguza watu waliokuwa
wanakosa hewa kwa kujazana wakati wakisibiri mkutano kuanza.
Mwenyekiti
wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho
Kikwete akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
wakati wa mkutano wa kampeni za CCM kwenye viwanja vya Jangwani..Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliofurika kusikiliza sera na mipango ya CCM .
Hii ndio Jangwani
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Ilala Mhe. Mussa Hassan Zungu kwenye mkutano mkubwa wa kampeni Jangwani, jijini Dar es Salaam.
Mke wa mgombea wa urais kupitia CCM Mama Janeth Magufuli akihutubia wakazi wa Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jangwani .
Post a Comment