Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar
kupitia CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Viongozi wa
Taasisi za Kiislamu katika ukumbi wa Baitul-Yamin, Malindi mjini
Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi wa Taasisi za Kiislamu Zanzibar wakimsikiliza Maalim Seif.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar
kupitia CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiitikia dua baada ya
mazungumzo yake na viongozi hao wa dini.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar
kupitia CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiagana na viongozi hao wa
dini baada ya mazungumzo yao.
(Picha na Salmin Said, OMKR)
Na: Hassan Hamad, OMKR.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameahidi
kushirikiana na taasisi zote za dini nchini sambamba na kuziendeleza
madrasa za Kur’an, ili ziendane na wakati uliopo.
Maalim
Seif ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi
CUF ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi wa taasisi za
Kiislamu katika ukumbi wa Baitul-Yamin Malindi mjini Zanzibar.
Amesema
Serikali atakayoiongoza iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar
itashirikiana kwa karibu na taasisi hizo ili kuona kuwa michango yao
inasaidia kuchangia juhudi za maendeleo na ustawi wa Zanzibar.
Amewataka
viongozi hao wa dini kudhibiti tofauti ndogo ndogo za kimadhehebu, ili
zisiwe chanzo cha kuvuruga umoja wa waislamu nchini.
Sambamba
na hilo Maalim Seif amesema bado madrasa za Kur’an hazijapewa umuhimu
unaostahiki, na kuahidi kulishughulikia suala hilo ili kuzijengea
mazingira bora na kuangalia maslahi ya walimu wa madrasa hizo.
Amesema
iwapo atachaguliwa kuongoza nchini, Serikali yake itatoa mchango wake
katika kuziendeleza madrasa ili ziwe za kisasa kwa kuzipatia mahitaji
yote ya msingi yakiwemo vikalio pamoja vifaa vya kusomea.
Amewakumbusha
walimu wa madrasa kuweka mbele maendeleo ya watoto kwa kuwajenga
kimaadili, ili waweze kuwa raia wema na viongozi bora wa baadae.
Mapema
akizungumza kwa niaba ya viongozi wa taasisi hizo za Kiislamu, Sheikh
Khamis Yussuf amesema taasisi hizo ziko tayari kuzungumza na
kushirikiana na kiongozi yeyote wa serikali kwa lengo kuweka mustakbali
mwema wa Zanzibar.
Amewaomba
viongozi wa Serikali kutoa ushirikiano katika kuulinda na kuuendeleza
utamaduni wa Zanzibar ili usiharibiwe na tamaduni nyengine, na kwamba
utamaduni ni rasilimali muhimu kwa taifa.
Wiki
iliyopita Maalim Seif alikutana na viongozi wa dini ya kikristo waliopo
Zanzibar katika kituo cha utengamano Welezo, kuzungumzia juu ya umuhimu
kutunza na kuilinda amani ya Zanzibar.
Post a Comment