Charles
Boniface Mkwasa amepewa mkataba wa kudumu kukinoa kikosi cha timu ya
Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu
kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu na kumalizika Machi 31, 2017.
TFF
Imefikia makubaliano hayo na kocha Mkwasa baada ya kurudhika na utendaji
wake katika kukinoa kikosi cha timu ya Taifa, ambapo mpaka sasa ameweza
kuingoza Stars katika sare ya michezo miwili dhidi ya Uganda na
Nigeria.
Kufuatia kusaini mkataba huo, Mkwasa atapatiwa huduma na marupurupu yote aliyokuwa akipewa kocha aliyeondoka.
Naye
kocha Mkwassa ameeleza kufurahishwa na makubaliano haya na ameahidi
kufanya kila jitihada kuhakikisha kiwango cha Timu ya Taifa kinapanda.
Aidha Kocha Mkwassa ametoa wito kwa wadau wa mpira kumpa ushirikiano katika majukumu yake mapya.
Post a Comment