THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
Uhuru Kenyatta wa Kenya amemshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa
juhudi na busara zake wakati nchi hiyo ilipoingia kwenye machafuko ya
kisiasa mwaka 2007.
Rais
Kenyatta amemshukuru Rais Kikwete leo mbele ya wafanya biashara wa
Kenya na Tanzania, wakati wakufungua Kikao cha wafanyabiashara pamoja
jijini Nairobi leo asubuhi.
"Kama
isingekua msaada wako mwaka 2007 na juhudi zako, historia ya Kenya leo
ingekua tofauti, asante kwa msaada wako na tunautambua urafiki wetu". Rais Kenyatta amemuambia Rais Kikwete.
Kenya
iliingia kwenye machafuko ya Kisiasa mwaka 2007 kufuatia Uchaguzi Mkuu
wa Nchi hiyo ambapo mapigano na machafuko yalisababisha vifo, uharibifu
wa mali na watu kukosa pahali pa kuishi na kusababisha kukimbia makazi
yao.
Rais
Kikwete aliombwa na Umoja wa Afrika kama mwanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki kusaidia katika juhudi za usuluhishi ambapo hatimaye,
pande mbili zilizokua zinazozana ziliunda serikali ya Umoja wa Kitaifa
ambayo ilileta utulivu na kusitisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Rais Kenyatta pia amemshukuru Rais Kikwete kwa juhudi zake kwenye uwekezaji na kwenye miundombinu ambayo inaimarisha Jumuiya.
Rais
Kenyatta pia ametambua na kupongeza juhudi za Rais Kikwete katika
kuhamasisha uwekezaji, biashara, miundombinu na uwekezaji kwa ujumla na
kueleza kuwa katika kipindi cha miaka 10 ya Rais Kikwete biashara na
mauzo ya Kenya Tanzania yameongezeka kwa asilimia 5.5 katika kipindi
hicho.
Nae
Rais Kikwete amesema anaamini biashara na uwekezaji baina ya Kenya na
Tanzania na Afrika Mashariki kwa Ujumla bado unaweza kuongezeka mara
tatu zaidi ya sasa.
Rais
Kikwete pia ametembelea makao makuu ya jiji la Nairobi na kupokelewa na
gavana wa Nairobi Dr. Evans Kidero ambapo amekabidhiwa ufunguo wa jiji
la Nairobi na pia kupata heshima ya kuzindua mtaa ulioko maeneo ya Ikulu
ambao umepewa jina la Jakaya Kikwete. Mtaa huo ulikua unajulikana kama
barabara ya Milimani.
Kabla
ya kumkaribisha Rais Kikwete kuzindua barabara hiyo Dr. Kidero amesema
Kenya inamshukuru Rais Kikwete kwa dhati na kwamba Ushirikiano wa
kibiashara na kijamii ni mzuri sana.
Rais
Kikwete anatarajia kuhutubia Bunge la Kenya baadae mchana na kuwaeleza
wananchi wote wa Kenya kuwa anatarajia kukabidhi madaraka kwa Rais
Mwingine baadae mwaka huu.
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Nairobi-Kenya
6 Oktoba, 2015
Post a Comment