Watanzania wametakiwa kutomchagua mgombea
urais wa CCM, Dk John Magufuli kwa madai kuwa Serikali
iliyopo madarakani inatumia mabilioni ya fedha kununua
fulana, kofia na kugawa bure, huku ikishindwa kuwalipia
chakula wanafunzi shuleni.
Wito huo ulitolewa jana na mgombea urais wa ACTWazalendo,
Anna Mghwira kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika
Uwanja wa Mbuzi uliopo mji wa Mugumu wilayani hapa Mkoa wa Mara.
Mghwira (pichani) alisema mfumo mbovu wa CCM na Serikali yake, umechangia huduma za jamii
kuuzwa na wanafunzi kukosa chakula shuleni.
Huku akishangiliwa na umati uliofurika kusikiliza sera za ACT Wazalendo, licha ya mvua
iliyokuwa ikinyesha, Mghwira alisema ni kipindi cha kuikataa CCM kwa kuwa haina uchungu na
wananchi, badala yake imekuwa ikiwakumbuka wakati wa uchaguzi kwa kuwapatia fulana na
kofia bure.
“Sasa hivi tisheti za njano na kofia zimetapakaa sana, wanagawa bure na kusomba watu kwa
malori ili wajae kwenye mikutano yao, wakati watoto wanakaa chini, hawapati chakula shuleni,
watumishi hawalipwi, dawa hospitali hakuna, barabara mbovu.
Ni kipindi cha kuwataka wapishe
Ikulu,” alisema.
Kuhusu
kauli za Magufuli kwamba Serikali yake itakuwa ya viwanda, alisema
anatakiwa kuwatajia Watanzania aliyeviuza viwanda 300 vilivyojengwa
Mwalimu Nyerere wakati wa uongozi wake.
Kuhusu ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, alidai kauli anazotoa mgombea huyo wa CCM
hazina ukweli kwa sababu barabara ya kutoka Bunda hadi Serengeti haifai kutoka na ubovu.
“Kwa zaidi ya miaka 15 wanawaahidi tu, wilaya hii yenye neema na jina kubwa ndiyo imesahaulika
hivi, wanathamini wanyama kuliko watu. Muikatae CCM mwaka huu,” alisema.
Post a Comment