Mkuu
wa mkoa wa Njombe Dr Rehema Nchimbi kulia akiwa na Deo Filikunjombe
mgombea ubunge jimbo la Ludewa na mbunge aliyemaliza muda wake
katikati kushoto ni msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis
Mutungi leo wakati wa mazishi ya Mchungaji Mtikila
Mchungaji Patrick Mgaya aliyekuwa safari moja na marehemu Mtikila wa pili kulia akiwa katika mazishi hayo
Waombolezaji wakiwa msibani
Filikunjombe akitoa salamu zake wakati wa mazishi ya Mtikila
Wananchi wakimsikiliza Filikunjombe
Filikunjombea akitoa mkono wa pole kwa wafiwa katikati ni mjane Mama Georgina Mtikila
Filikunjombe akiwasili msibani kwa chopa
Jaji Francis Mutungi kushoto Bw MGaya na Askofu Mtetemela na Filikunjombe wakiwa msibani
Filikunjombe akijiandaa kubeba jeneza
Mjane wa Mtikila akiweka shada la maua
MWENYEKITI wa chama cha DP mchungaji Christopher Mtikila amezikwa kijijini kwake Milo Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe leo.
Vilio
vyatawala huku aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na
Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi watao ya Moyoni
wasema alikuwa kiungo mhimu katika Taifa .
Wakati
Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Mutungi akiwataka watanzania
hasa viongozi wa vyama vya siasa kumuenzi Mchungaji Mtikila kwa kuenzi
Amani wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu octoba 25 mwaka huu
,Filikunjombe asema mbali ya ukorofi wa Mtikila kwa kile alichokiamini
ila kwake alikuwa ni mshauri mkubwa wa Ubunge wake katika jimbo la
Ludewa.
Wakitoa
salamu za rambi rambi wakati wa mazishi hayo yaliyofanyika leo
kijijini kwake Milo Wilaya ya Ludewa ,Jaji Mutungi alisema kuwa katika
enzi za uhai wake marehemu Mtikila alikuwa akisimamia kile
anachokiamini.
Alisema
kuwa mbali ya misimamo yake ya kusimamia alichokiamini bado alikuwa ni
mtu wa kujenga hoja na ambae hakupenda kuhatarisha Amani ya nchi hakuwa
anapenda njia za mkato katika kupata majibu ya kile asichokiamini.
"
Njia za mkato marehemu hakupenda kabisa kwani hata Kama jambo la
kutisha ambalo wengine huogopa yeye alikuwa tayari kwenda mahakamani
kusaka Haki yake bila kuhatarisha Amani ya nchi Mimi nafikiri kila mmoja
akafuata misingi yake katika kudai Haki bila kuvuruga amani naamini
tutafanikiwa.
"
Alisema kuwa kuna mapungufu yanaweza kujitokeza ila Jambo la msingi
kila mmoja kutanguliza kwanza amani ya nchi badala kuipa kisogo Amani na
kupenda machafuko katika nchi".
Hivyo aliwataka watanzania bila kujali itikadi zao za vyama kuendelea na siasa huku wakitanguliza Amani ya nchi.
Mbunge
aliyemaliza muda wake wa jimbo la Ludewa ambae ni mgombea Ubunge wa
jimbo hilo Bw Filikunjombe alisema kuwa pamoja na Mchungaji Mtikila enzi
za uhai wake alisimamia jambo ambalo
alikuwa akiamini ila kwake amekuwa msaada mkubwa katika ushauri wa kuwatumikia wananchi wa Ludewa .
Alisema
Mchungaji Mtikila hakuwa tayari kumuunga mkono mbunge wa Ludewa ambae
hakuwa msaada wa kimaendeleo kwa wananchi ila kwa upande wake alikuwa
akimuunga mkono na hata kutosimamisha mgombea katika jimbo la Ludewa.
"
Mchungaji Mtikila hakuwa tayari kuungana na mbunge asiyefanya Kazi za
maendeleo jimboni Ludewa ila kwangu alikuwa akiniunga mkono na hata
kunipingeza kwa Kazi nzuri ..... Kicho chake ni pigo kubwa kwa Taifa
hasa kwa wana Ludewa ambao tulijivunia sana uwepo wake"
Hata
hivyo alisema njia pekee kwake ya kumuenzi Mchungaji Mtikila ni
kuendelea kuwatumikia vema wananchi wa Ludewa kwa kuleta maendeleo zaidi
Kama alivyohitaji katika uhai wake.
Filikunjombe
alisema katika kuamini kwake na kusimamia anachokiamini hadi mauti
inamkuta alikuwa akitetea kuwepo kwa nchi ya Tanganyika na ndio maana
kazikwa na bendera ya Tanganyika na kudai kuwa hakuna na kosa kupigania
Tanganyika kwani Tanganyika inahitajika.
Mkuu
wa Mkoa wa Njombe Dr Rerema Nchimbi alisema kuwa Mkoa wa Njombe
umepoteza kiongozi makini na kuwa katika kumuenzi ni vema kwa vyama vya
siasa kuendesha kampeni za amani na utulivu zaidi na kuwa wakati taifa
linaelekea katika uchaguzi mkuu ni vema kila chama kumuenzi Mtikila kwa
kulinda Amani .
Naibu
Katibu mkuu wa DP Taifa Abdul Mluya alisema kuwa suala la kifo cha
mwenyekiti wake ni utata mtupu na bado wanaendelea kuchunguza.
Wakati
huo huo Chopa ya Filikunjombe aliyotumia kufaria kwenda katika mazishi
hayo iliwafanya wananchi kuacha kusikiliza Salam mbali mbali za viongozi
na kukimbilia kutazama na kumlaki Mgombea huyo Ubunge jimbo la Ludewa.

Post a Comment