Mkurugezi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu wa NBS, Ephraim Kwesigabo (kushoto), akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo
kuhusu, Fahirisi za bei za Taifa kwa mwezi Septembva, 2015.
Taarifa ikichuliwa na wanahabari.
Mwanahabari Hilda kutoka gazeti la Daily News akichukua taarifa hiyo kwa umakini zaidi.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
OFISI ya
Taifa ya Takwimu (NBS) imesema mfumuko wa bei umeshuka hadi asilimia
6.1 kwa Septemba kutoka asilimia 6.4 kwa kipindi cha Agost 2015.
Akizungumza
Dar es Salaam leo Mkurugezi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu wa
NBS, Ephraim Kwesigabo alisema kushuka kwa mfumuko wa bei kunachangiwa
na kushuka kwa bidhaa za vyakula zinazotumiwa majumbani na kwenye
migahawa pamoja na vinywaji baridi.
Alisema
mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa Septemba 2015
umepungua hadi kufikia asilimia 9.6 kutoka aslimia 10.2 kwa Agost 2015
''Bidhaa
za huduma kwa mwaka huu Septemba umepungua ikilinganishwa na kiasi cha
bei kilichokuwepo Agost mwaka uliopita ambapo farihisi za bidhaa
zimeongezeka hadi 159.4 na kutoka 149.93 Septemba 2014,' alisema.
Kwesigabo
alisema mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka unapima unapima kiwango cha
badiliko la kiasi cha bei za bidhaa pamoja na huduma zote zinazotumiwa
na kaya binafsi.
''Mfumuko
wa bei ambao haujumlishi bei za vyakula na na nishati umebakia kuwa
asilimia 22 kwa Septemba 2015 kama ilivyokuwa Agost 2015,''alisema
Alisema
thamani ya shilingi inatafsiriwa katika matumizi ya mlaji wa bidhaa
mbalimbali ambapo shilingi ya Tanzania imeonekana kununua bidhaa na
huduma zilezile katika vipimo tofauti tofauti.
''Uwezo
wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma imefikia
shilingi 62 na senti 88 kwa Septemba 2015 kutoka Septemba
2010,''alisema.
Mkurugezi
huyo alisema farisihi za nishati na mafta zimekuwa na mwendendo wa hali
ya juu kwa kipindi chote zikilinganishwa na farihisi nyingine.
Alisema
mfuko wa bei kwa kipindi cha mwezi mmoja umeongezeka kwa aslimia 0.1
ukiwa umechangiwa na baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula kama vile
mkaa,pamoja na huduma za saluni.
Post a Comment