Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akizungumza na
vyombo vya habari jinsi alivyomfahamu aliyekuwa waziri wa Viwanda na
Biashara, marehemu Dk Abdallah Kigoda wakati wa mapokezi ya mwili kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dcar es Salaam jioni hii, ukitokea
India ambako alipatwa na mauti.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA
WA MATUKIO BLOG
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, na
Mgombea ubunge Jimbo la Handeni kupitia CCM, marahemu Dk Abdallah
Kigoda, ukihamishiwa kwenye gari lingine wakati wa mapokezi ya mwili huo
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam
jana, ukitokea nchini India ambako alipatwa na mauti. Mwili huo
ulikwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, kusubiri kuagwa leo
katika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam
Dk Magufuli akimfariji mtoto wa marehemu Dk Kigoda kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha Rose Migiro akimfariji dadake na
marehemu Dk Kigoda, Dk Aisha Kigoda..PICHA ZOTE NA RICHARD
MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Dk Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue
wakati wa mapokezi ya mwili wa marehemu Dk Kigoda Uwanja wa Ndege.
Dk
Magufuli (kulia) akiangalia jeneza lenye mwili wa Dk Kigoda ukishushwa
wakati wa mapokezi ya mwili huo kwenye Uwanja wa Ndege, Dar..PICHA ZOTE
NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli naye yupo kuungana na Watanzania wengine kuupokea mwili wa Kigoda. Aliyekuwa
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda
akijumuika na Watanzania wengine kuupokea mwili wa marehemu Kigoda.
Ndugu, Jamaa na marafiki wakiusubiri kuupokea mwili.Hali ya majonzi ikitawala eneo loa Uwanja wa Ndege wa Mwl. Julius Nyerere Dar.
Mwili wa
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda aliyefariki juzi
katika hospitali ya Appolo nchini India alikokuwa amelazwa kwa matibabu,
umewasili leo jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius
Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ndege ya Shirika la Emirates.
Mwili wa Waziri Kigoda utaagwa kesho viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Post a Comment