Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva amejibu malalamiko yaliyotolewa na viongozi wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, kuhusu utofauti kati ya baadhi ya matokeo yanayotangazwa na Tume hiyo na yale yaliyokuwepo vituoni.
Akiongea
hivi punde kabla ya kuanza kutangaza matokeo mengine ya majimbo 54,
Jaji Lubuva amekanusha taarifa zilizotolewa jana na viongozi wa Ukawa na
kutolea ufafanuzi matokeo ya nafasi ya urais yanayopokelewa na
kutangazwa na Tume hiyo.
Hivi ndivyo alivyoeleza:
“Tusingependa
wakati huu kulumbana na vyama vya siasa au wadau wengine. Hiyo ndiyo
nia yetu. Lakini pale panapokuwa na upotoshaji wa hali ya juu, Tume
inalazimika kusema machache.
"Moja ni upotoshaji unandelea sasa hivi kwamba Tume ya Uchaguzi, matokeo tunayosoma hapa yamechakachuliwa kuhusu wagombea wa urais.
"Hiyo sio kweli hata kidogo, ningependa kutumia nafasi hii kupitia ninyi waandishi wa habari kuelewesha wananchi kwamba wasipotoshwe.

Post a Comment