1Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhelm Meru akizungumza na waajiriwa wapya katika
Ufunguzi wa Semina Elekezi iliyofanyika
katika Chuo cha Taifa cha Utalii
Kampasi ya Temeke, jijini Dar es
salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Idara Rasilimali watu Bw. Said Msambachi (
wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali watu Bi.
Aurelia Matagi , ( wa kwanza kushoto) , Kwa upande wa kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Bw. Zahoro
Kimwaga pamoja Mkurugenzi wa Idara ya
Wanyamapori Bw. Herman Keryaro
Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali watu Bi Aurelia Matagi
( kulia) akiwa na Afisa Utumishi Mwandamizi
Bw. Safari, wakiwa wanatoa maelekezo ya kujaza fomu za kuajiriwa
katika Semina Elekezi iliyofanyika
katika Chuo cha Taifa cha Utalii
Kampasi ya Temeke, jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Watumishi wapya walioajiriwa na Wizara ya Maliasili na Utalii
wakiwa katika Ufunguzi wa Semina Elekezi ya Waajiriwa wapya iliyofanyika
katika Chuo cha Taifa cha Utalii
Kampasi ya Temeke, jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Bw. Herman Keryaro (
kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali
watu Bw. Said Msambachi ( kulia) mara baada ya Katibu Mkuu, Dkt. Meru
kuwasili katika ufunguzi wa Semina Elekezi ya waajiriwa wapya iliyofanyika
katika Chuo cha Taifa cha Utalii
Kampasi ya Temeke, jijini Dar es
salaam.
WIZARA YA MALIASILI NA
UTALII YAAJIRI WATUMISHI WAPYA 588
Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa ajira
mpya kwa Watumishi wapya wapatao 588 ikiwa idadi kubwa miongoni mwao ni
Watumishi wa kada ya Afisa Wanyamapori na Wahifadhi wanyamapori lengo likiwa ni kukabiliana na
mashambulio mengi kutoka kwa majangili.
Akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo elekezi kwa waajiliwa
wapya hao yaliyofanyika leo katika Chuo
cha Taifa cha Utalii katika Kampasi ya Temeke
jijini Dar es Salam, Katibu Mkuu
wa Wizara ya Maliasili na Utalii , Dkt. Adelhelm Meru amesema watumishi hao ni lazima wajitume ili
kukidhi malengo kwa kudhibiti na kusimamamia matumizi endelevu ya wanyamapori
pamoja na kuzuia uharibifu wa mazingira ya mapori ya akiba.
‘’Fursa hii mliyoipata isaidie kuongeza
chachu na ufanisi katika kutekeleza majukumu ya Wizara kwa kuhakikisha kuwa
Maliasili tulizonazo zinalindwa na kutunzwa kikamilifu kwa manufaa ya kizazi
cha sasa na cha baadaye’’ Dkt. Meru alisisitiza.
Amewataka watumishi hao kufanya doria
katika maeneo ya mapori ili kuimarisha uwepo wa Wanyamapori katika maeneo ambayo
Watalii wanaweza kupata fursa ya kuwaona kwa urahisi zaidi.
Aliongeza kuwa Watumishi hao ni lazima waweke nguvu na mikakati endelevu katika
kupambana na uchomaji moto ovyo wa mapori, kilimo na uingizaji wa mifugo katika
maeneo ya mapori yaliyotengwa kwa ajili ya Wanyamapori
Pia aliwataka Watumishi hao kujiepusha na
na tabia ya kupokea rushwa hasa kwa watumishi walio kwenye Mapori ya akiba, mapori tengefu na vituo
vingine vya kazi na Mtumishi yeyote atakayethibitika kupokea rushwa
atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kupoteza ajira yake.
Aidha, Dkt. Meru amewaasa watumishi wapya
kujiepusha na anasa na ulevi wa kupindukia likiwemo janga la Ukimwi ambalo limekuwa sio rafiki kwa nguvu kazi ya taifa ambayo imepatikana
kwa gharama kubwa
Watumishi wapya wapatao 588 walioajiriwa ni
Maafisa wanyamapori daraja la pili 111, Maafisa Utalii daraja la pili 17, Wahifadhi wanyamapori daraja la pili 14, Wahifadhi Wanyamapori la pili tatu 433.
Wengine ni Wahasibu wasaidizi 11,
Msaidizi wa Maktaba 1 na fundi sanifu Umeme 1, Mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika kwa muda
wa siku tatu.
katika idara mbalimbali wakiwemo, wahifadhi
wa wanyamapori daraja la (2) 14, wahifadhi wanyamapori daraja la (3) 433
uhasibu wasaidizi 11, fundi umeme 1, maofisa utalii daraja la (2) 17, msaidizi
wa Maktaba 1, leo Asubuhi katika ghafla ya kuwa karibisha na kuwapa mafunzo
waajiliwa hao iliyofanyika jijini Dar es salaam katika chuo cha utalii
kilichopo Temeke. Dkt. Meru alisema, rushwa ni tatizo kubwa katika Taifa letu
hivyo Wizara ya Maliasili na Utalii haina budi kuwa mfano wa kuigwa katika
kupiga vita rushwa na kutatua matatizo ya wafanyakazi hasa kwa watumishi walio
kwenye Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu na vituo vingine vya kazi.
Pia aliongezea nakusema, napenda nimalizie
kwa kuzumzia kwa kifupi tatizo lingine linalokabili Taifa letu, Tatizo hili ni
janga la ukimwi. Uboreshaji wa utendaji kazi katika utumishi wa Umma hususani ulinzi
wa Wanyamapori hauwezi kufanikiwa ikiwa janga la Ukimwi halitadhibitiwa. UKIMWI
unasababisha vifo vya watumishi hivyo kulipunguzia Taifa nguvu kazi ambayo
imepatikana kwa gharama kubwa, kwa hiyo kila mmoja wenu anatakiwa ashiriki
kikamilifu katika kujikinga na janga hilo na kuchukua tahadhari kupunguza kuenea kwa ugonjwa huu. Wizara
itaendelea na jukumu lake la kuelimisha wafanyakazi kuhusu mapambano dhidi ya
UKIMWI.
Pia mmoja wa waajiliwa hao nae alimshukuru
katikbu Mkuu kwaniaba ya waajiliwa wenzake na kuahidi kuwa watafanya kazi
kikamilifu, watakuwa waadilifu na watashirikiana na wafanyakazi wengine wa
Wizara ya Maliasili na Utalii.
Post a Comment