Amiri
Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Mkuu wa Majeshi
ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange vitabu kwaajili ya Chuo Cha ulinzi
cha Taifa National Defence College(NDC) katika hafla fupi iliyofanyika
ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho cha NDC Meja
Jenerali Gaudence Milanzi.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue,Mkuu
wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange,Mkuu wa Chuo Cha NDC
Meja Jenerali Gaudence Milanzi wakiangali baadhi ya vitabu ambavyo Rais
ameviakbidhi kwaajili ya matumizi ya Chuo hicho.
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Katibu mkuu kiongozi Balozi
Ombeni Sefue(watatu kushoto),Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis
Mwamunyange,(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Ulinzi Cha Taifa(NDC) Meja
Jenerali Gaudence Milanzi(kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na
viongozi waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania muda mfupi baada ya
Rais Kikwete kukabidhi vitabu kwaajili ya National Defence College)
katika hafla iliyofanyika ikulu jijijini Dar es Salaam leo.
(Picha na Freddy MRO)
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete leo Jumatatu Oktoba 26, 2015, amelikabidhi Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vitabu kwa ajili ya vyuo vyake
na maktaba zake, ikiwa ni mara ya tano kwa Rais Kikwete kulikabidhi
Jeshi hilo vitabu wakati wa uongozi wake.
Vitabu
hivyo 384 vilivyokabidhiwa leo vitatumiwa na Chuo cha Ulinzi wa Taifa
cha National Defence College (NDC) na wanafunzi wanaosoma katika Chuo
hicho chenye hadhi ya kimataifa.
Mkuu
wa Chuo hicho, Meja Jenerali Gaudence Milanzi amehudhuria sherehe ya
makabidhiano ya vitabu hivyo ambavyo Rais Kikwete amevikabidhi kwa Mkuu
wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange katika sherehe fupi iliyofanyika
Ikulu, Dar es Salaam.
Hiyo
ni mara tano kwa Rais Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu kukabidhi vitabu kwa
JWTZ katika azma yake ya kuboresha vyuo na maktaba ya vyuo hivyo vya
Jeshi. Mpaka sasa, Rais Kikwete amekwisha kabidhi vitabu 3,136 kwa
Jeshi.
Rais
Kikwete aliahidi kulinunulia na kulikabidhi Jeshi vitabu (titles) mbali
mbali 503 na kufuatia makabidhiano ya leo, sasa vimebakia vitabu
(titles) 27 ambavyo navyo tayari vimenunuliwa na vinasubiriwa
kusafirishwa kuletwa nchini kutoka vilikonunuliwa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
26 Oktoba, 2015
Post a Comment