Stanslaus Mabula akiongea na wanahabari baada ya kutangazwa mshindi wa Ubunge Jimbo la Nyamagana (CCM)
Na:George Binagi-GB Pazzo
Mgombea
wa Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza ameibuka
mshindi wa kiti cha Ubunge katika jimbo hilo kwa kupata kura 81,017 na
hivyo kumbwaga aliekuwa mbunge wa jimbo hilo Ezekiel Wenje kutoka Chama
cha Demokrasia na Maendeleo Chadema aliepata kura 79,280.
Matokeo
hayo yalitangazwa na Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Jimboni humo ambae pia
ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Tito Mahinya huku kukiwa na Ulinzi
Mkali wa vyombo vya ulinzi na usalama katika viunga vya ofisi za Jiji
hilo.
Akitakangaza
matokeo hayo majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo, Mahinya
alibainisha kuwa pia CCM imeibuka kidedea kwa upande wa Madiwani ambapo
kati ya Kata 18, imeshinda Kata 14 na Chadema Kata Nne.
Kwa
upande wa Wagombea wengine, Chacha Okong’o (ACT Wazalendo) alipata kura
161, Faida Potea (CUF) amepata kura 1,005, Ahmad Mkangwa (NRA) kura
104, Mohamed Msanya (Jahazi Asilia) kura 175 na Ramadhan Mtoro (UDP)
amepata kura 68.
Hata
hivyo kabla ya matokeo hayo kutangzwa, Mgombea kutoka Chadema Ezekiel
Wenje alikataa kusaini karatasi ya wagombea na kubainisha kuwa
demokrasia haikutumika katika zoezi zima la uhesabuji wa kura katika
uchaguzi huo na kwamba atafuata hatua zaidi za kisheria katika kupinga
matokeo hayo.
Kwa
upande wake Mshindi wa Uchaguzi huo Stanslaus Mabula alisema kuwa tangu
awali alitarajia ushindi huo na kwamba suala la demokrasia
limezingatiwa.
Katika
hatua nyingine Mabula alibainisha kuwa atahakikisha anatatua changamoto
zinazolikabili Jiji la Mwanza ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha wakazi
wa Jiji katika shughuli mbalimbali za uzalishaji ili waweze kujitegemea
kiuchumi.
Ezekiel Wenje akiongea na wanahabari muda mfupi kabla ya matokeo kutangazwa
Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Jijini Mwanza Titho Mahinya akitangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu Jijini Mwanza
Kushoto
ni Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana akiwa na Katibu wa CCM Mkoa wa
Mwanza Miraji Mtaturu (kulia) muda mfupi kabla ya matokeo kutangazwa
BINAGI MEDIA GROUP, KWA PAMOJA TUIJUZE JAMII
Post a Comment