Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wabunge Walioingia, Waliotoka Hawa hapa .....


Anne Kilango Malecela.

Profesa Jumanne Maghembe. 

Stori: Oscar Ndauka
TAYARI! Moshi mweupe umeanza kuonekana kwenye matokeo ya uchaguzi mkuu wa udiwani, ubunge na urais wa vyama zaidi ya 20 uliofanyika nchini kote, Oktoba 25, mwaka huu, Uwazi linatiririka.

Vyama hivyo kwenye mabano na wagombea wao wa urais ni Anna Mghwira (ACT-Wazalendo), Hashim Rungwe (Umma), John Magufuli (CCM) na Edward Lowassa (Chadema akiungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi, Ukawa ambao Cuf, NCCR-Mageuzi na NLD).
Wengine ni Macmillan Lyimo (TLP), Lutasola Yemba (ADC), Jankin Kasambala (NRA) na Fahim Dovutwa (UPDP).
Matokeo ya ubunge na udiwani ndiyo yanayotikisa mpaka sasa huku kura za urais, wagombea wake wakuu, Dk. Magufuli na Lowassa wakiendelea kukimbizana sehemu nyingine kwa mbali, nyingine kwa karibu.
HAWA WAMETOKA
Baadhi ya wabunge wameikanyaga siku ya jana kwa vilio kufuatia kura zao kutotosha kwenye majimbo hivyo kutoingia bungeni msimu ujao.Wabunge hao ambao wengine ni vigogo ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri (CCM-Jimbo la Siha) na Highness Kiwia (Chadema-Ilemela), Agustine Mrema, TLP (Vunjo), Balozi Khamis Kagasheki (CCM-Bukoba Mjini).
Wengine ni aliyekuwa Waziri wa Uwezeshaji na Uwezekaji, Christopher Chiza (CCM-Buyungu), aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Chakula, Steven Wassira (CCM-Bunda Mjini), aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Kebwe Steven Kebwe (CCM-Serengeti) na Anne Kilango Malecela wa CCM-Same (pichani kulia).
HAWA WAMEINGIA
Wagombea wanaocheka ni wale ambao wamerudi na ambao walikuwepo bungeni msimu uliopita ambao ni Zitto Zubeir Kabwe, Kigoma Mjini (ACT-wazalendo), Joshua Samuel Nassari, Arumeru Mashariki (Chadema), Vedasto Mathayo, Musoma Mjini (CCM), Ridhiwani Kikwete (CCM-Chalinze), Sylvester Koka (CCM-Kibaha Mjini), Ahmed Shabiby (CCM-Gairo), Suleiman Saddiq (CCM-Mvomero).
Wengine ni Juma Nkamia (CCM-Chemba), Omar Badwel (CCM-Bahi), George Simbachawene (CCM-Kibakwe), George Lubeleje (CCM- Mpwapwa), Livingstone Lusinde (CCM-Mtera), Antony Mavunde (CCM-Dodoma-Mjini), Constatine Kinyau (CCM-Geita Mjini) na Joseph Kasheku Msukuma (CCM-Geita Vijijini).
Wengine walioingia kwenye bunge lijalo ni Hussein Bashe (CCM-Nzega Mjini), Hamis Kigwangala (CCM-Nzega Vijijini), Mwigulu Mchemba (CCM-Iramba Mashariki), Lazaro Nyalandu (CCM- Singida Kaskazini), Prof. Sospeter Muhongo (CCM-Musoma Vijijini), Suleiman Jafo (CCM-Kisarawe), Angelina Mabula (CCM- Ilemela), Jumanne Kishimba (CCM-Kahama), Mohamed Abood (CCM-Morogoro Mjini), Januari Makamba (CCM-Bumbuli), Musa Hassan Zungu (CCM-Ilala), Hassan Masara (CCM- Nachingwea), Ally Kessy (CCM-Nkasi Kaskazini), Jumanne Mwaijage (CCM-Muleba Kaskazini) na Sebastian Kapufi (CCM-Mpanda Mjini).
Kwa jana, CCM walionekana kuongoza kwenye majimbo mengi, kwani wengine ambao ni wa CCM wameingia bungeni ni Selemani Kakoso (CCM-Mpanda Vijijini), Issac Kamwele (CCM- Katavi), Richard Mbogo (CCM-Nsimbo), Leonidas Gama (CCM- Songea Mjini), Eng. Stella Manyanya (CCM-Nyasa), Ramo Makani (CCM- Tunduru), Daimu Mpakate (CCM-Tunduru Kusini) na Jenister Mhagama (CCM-Peramiho).
Wengine ni Joseph Mhagama (CCM-Madaba), Sixtus Mapunda (CCM-Mbinga Mjini), Diodorus Kamala (CCM-Nkenge), Job Ndugai (CCM-Kongwa), Sanda Edwin (CCM- Kondoa), Ashatu Kajaji (CCM- Kondoa), Rashid Shangazi (CCM-Mlalo), Jumaa Aweso (CCM-Pangani) na Omar Kigua (CCM- Kilindi).
Pia wamo Danstan Kitandula (CCM-Mkinga), Mboni Mhita (CCM-Handeni Vijijini), Adadi Rajabu (CCM- Muheza), Mary Chatanda (CCM-Korogwe Mjini), Stephen Ngonyani ‘Maji Marefu’ (CCM-Korogwe Vijijini), Ester Bulaya (Chadema-Bunda Mjini), Marwa Ryoba (Chadema-Serengeti) na Alfred Rwakatare (Chadema-Bukoba Mjini). Wengine ni William Ngeleja (CCM-Sengerema), Charles Tizeba (CCM-Buchosa) na Constantine Kanyasu (CCM-Geita Mjini) na Jumanne Maghembe (CCM-Mwanga).
Mpaka tunakwenda mitamboni mapema, majimbo ambayo matokeo yalikuwa yakisuasua ni Kinondoni, Ubungo, Kibamba, Temeke, Kawe, Kigamboni, Mbagala, Segerea na Ukonga. Majimbo yote haya ni ya Mkoa wa Dar es Salaam.
PIGA NIKUPIGE
Uchunguzi zaidi uliofanywa na gazeti hili ulibaini kuwa, CCM imefanikiwa kukomboa baadhi ya majimbo, hasa yale yaliyokuwa na upinzani mkuu kama Ilemela na Nyamagana jijini Mwanza.
Hata hivyo, upinzani nao wameonekana kuchukua baadhi ya majimbo mapya kama vile Bunda Mjini ambalo lilikuwa chini ya Wassira zamani. Ester Matiku amelitwaa Jimbo la Tarime (Chadema) ambalo awali lilikuwa la CCM.

GPL
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top