Rais
wa jamhuri ya muungano wa Tanzania anayemaliza muda wake Dr Jakaya
Kikwete amewahakikishia watanzania uchaguzi utakuwa huru na wa amani na
wasiwe na hofu, na kuwaonya wale ambao wanapanga kuleta fujo watakiona.
Rais
Kikwete ambaye pia ni mweyekiti wa CCM ametoa tahadhari hiyo hapa
Chakechake Pemba wakati akiwahutubia umati wa wanachama wa CCM na
wananchi waliofika katika uwanja wa Gombani ya kale katika mkutano wa
mwisho kwa Pemba wa kampeni ya mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi
ya CCM ambapo amesema yeye bado ni amiri jeshi mkuu wa nchi na kuwataka
watanzania kwenda kwa wingi kupiga kura.
Naye
mgombea urais wa Zanziabr Dr Ali Mohamed Shein katika mkutano huo
amewahidi wazanzibari kuwa ahadi alizozitoa katika mikutano ya kampeni
zake atahakikisha anazitekleza kwa vile yamo ndani ya ilani ikiwa ni
pamoja na umarishaji wa miundombinu na kuwapatia sekta ya uvvi vifaa na
boti za kisasa.
Katika
mkutano huo mkubwa wa aina yake kufanyika kiswani Pemba na kuhudhuriwa
karibu na viongozi wote wa juu wa SMZ ambapo pia mgombea mwenza wa urais
wa mungano Mhe Samiha Suluhu aliwaakikishia watanzania hasa walemavu na
wazee kuwa serikali ya CCM itawawekea mazingira mazuri ya maisha yao.
Post a Comment