Katibu
Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma Balozi Ombeni Sefue
akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete orodha ya zawadi mbalimbali
kutoka katika taasisi za umma wakati wa sherehe ya watumishi wa umma
kumuaga Rais iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es
Salaam jana.
Mkurugenzi
Mkuu wa TAKUKURU Dkt.Edward Hosea kwa niaba ya watumishi wa Umma
akimkabidhi Tuzo Maalum Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua
mchango wake katika kuboresha Utumishi wa Umma nchini wakati wa sherehe
ya Watumishi wa Umma Kumuaga Rais iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani
City jijini Dar es Salaam jana usiku.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Bwana Awadh Masawe akimkabidhi Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mfano wa ufunguo wa trekta alilokabidhiwa na
watumishi wa taasisi za umma jana wakati wa sherehe za kumauaga Rais
katika ukumbi wa Mlimani City jana.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete,Katibu Mkuu
Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma Balozi Ombeni Sefue,Jaji Mkuu
Othman Chande,Mwanasheria Mkuu Mh.George Masaju pamoja Katibu Mkuu Ofisi
ya Waziri Mkuu Bwana Florence Turuka wakiwa katika picha ya pamoja na
Makatibu wakuu wa Wizara Mbalimbali wakati wa Sherehe ya Watumishi wa
Umma Kumuaga Rais iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar
es Salaam jana.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia viongozi na wawakilishi wa
Watumishi wa Umma katika ukumbi wa Mlimani City wakati wa Sherehe ya
Watumishi wa Umma Kumuaga Rais jana.
(Picha na Freddy Maro).
Post a Comment