2.0
Taarifa hii si ya ukweli na ni ya upotoshaji,Mhe Jaji Mkuu hajawahi
kuzungumzia chochote kuhusu sheria hiyo ukitilia maanani kesi hiyo iko
Mahakama Kuu shauri Namba 37 ya 2015 iliyofunguliwa na Bi. Amy Kibatala
dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Mkurugenzi wa Uchaguzi
(DE) na itatolewa maamuzi kati ya tarehe 22 au 23 mwezi huu. Hivyo, kwa
mujibu wa sheria Mhe.Jaji Mkuu asingeweza kuzungumzia chochote kuhusu
sheria hiyo kwa kuwa suala hilo likoMAHAKAMANI.
3.0 Tulimwandikia Mkurugenzi wa Habari MAELEZO nakala
East Africa Television na kufuatilia kwenye Baraza la Habari (Media
Council) kuomba maelezo ya kina na usahihi wa taarifa hiyo, tarehe
21/10/2015 tumepokea barua Kumb Na EATV/ADMN/096/10/2015 ilyosaniwa
na Bi Regina Mengi Mkurugenzi Mtendaji wa East Africa Television
akiomba msamaha kuhusu taarifa hiyo potofu na kuwa watatoa maelezo ya
ziada kuwa, taarifa hiyo haikutolewa na Mhe.Jaji Mkuu wa Tanzania
Tunashukuru
kwa ushirikiano mkubwa tulioupata toka uongozi wa juu kabisa wa East
Africa Television kwa kuomba radhi mapema na Tunamini kuwa, vyombo vya
Habari na Wananchi kwa ujumla vitasitisha usambazaji wa taarifa hii
iliyokuwa si sahihi.
Barua ya kuomba radhi imeambatanishwa:
Imetolewa na:
MTENDAJI MKUU WA MAHAKAMA
Post a Comment