Serikali jijini Dar es Salaam imeagiza baa zote zinazouza pombe mpaka asubuhi kusitisha shughuli hiyo mkesha wa siku ya uchaguzi ili kuimarisha usalama Jumapili ijayo.
Aidha,
imesisitiza kwamba kila mwananchi atakayekwenda kupiga kura ahakikishe
anarudi nyumbani baada ya shughuli hiyo badala ya kukaa katika vikundi
kusubiri matokeo vituoni.
Agizo
hilo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki,
katika ibada maalum ya kuliombea Taifa amani na mvua, iliyoendeshwa na
Askofu Charles Gadi wa Kanisa la Huduma ya Good News for All Ministry,
jijini Dar es Salaam jana.
Askofu
Gadi katika maombi yake alisisitiza suala la amani na kumuomba Mwenyezi
Mungu alete mvua ili mabwawa yanayozalisha umeme yajae maji nishati ya
umeme ipatikane nchini kwa uhakika.
Post a Comment