Kura halali zitakazopigwa siku ya Jumapili kwa ajili ya kuwachagua viongozi kwenye Uchaguzi Mkuu zinaweza kuharibika ikiwa hazitapigwa kwa usahihi na kuondoa utata.
Kura iliyoharibika ni ile ambayo:
- Haina alama yoyote
- Imepigwa kwa wagombea zaidi ya mmoja
- Imeandikwa jina la mpiga kura
- Alama imewekwa nje ya kisanduku cha picha ya mgombea
- Haina muhuri wenye alama rasmi
Kura sahihi;
- Yenye alama ya ‘v’ kwenye kisanduku
- Yenye alama yoyote kwenye kisanduku/picha/ jina la mgombea
- Kutakuwa na utata endapo utaweka alama iliyopitiliza kisanduku cha mgombea mmoja na kufika kwa mwingine. Epuka kuharibu kura. Kura yako, mustakabali wako
Post a Comment