Mbunge mteule wa Jimbo la Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema
chama hicho kitahakikisha kinampata meya mpya mwenye uwezo wa kusimamia miradi ya maendeleo inayopangwa kila mwaka.
Sugu aliyasema hayo jana, wakati akizungumzia mikakati ya Chadema baada ya kupata ushindi
katika kata 26 kati ya 30 za jimbo lake.
“Tutamchagua meya atakayezuia mianya yote ya rushwa
na uonevu pamoja na kusimamia sheria rafiki na siyo kandamizi,” alisema Sugu.
Alisema
Mbeya itakuwa mfano wa kuigwa na majiji mengine ndani na nje ya nchi
kutokana na mpangilio utakavyokuwa katika kutatua kero ambazo zilikuwa
kikwazo kikubwa cha maendeleo
kwa wananchi.
Diwani mteule wa Kata ya Isanga, Anyandwile Mwalwiba, alisema wamejipanga kumpata meya
atakayekuwa tayari kuendana na kasi kubwa ya maendeleo na kulibadilisha Jiji la Mbeya.
Post a Comment