JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
“PRESS RELEASE” TAREHE 12.10.2015.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
MTU MMOJA MKAZI WA NZOVWE JIJINI MBEYA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA MALI YA WIZI.
MTU
MMOJA MKAZI WA NZOVWE JIJINI MBEYA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA BARAKA
SHANSIYA (26) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA
KIPANDE KIMOJA CHA SHABA MALI AMBAYO NI YA WIZI.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 11.10.2015 MAJIRA YA SAA 05:00 ALFAJIRI HUKO
ENEO LA SONGWE – DARAJANI, KATA YA SONGWE, TARAFA YA USONGWE, NJE
KIDOGO YA JIJI LA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA.
INADAIWA
KUWA, MTUHUMIWA AKIWA NA MWENZAKE WALIIBA VIPANDE VIWILI VYA SHABA
KUTOKA NDANI YA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.914 BPA/T.277 DET AINA YA
SCANIA BAADA YA KUKATA TURUBAI NA CLAM NA KISHA KUIBA. GARI HILO
LILIKUWA LIKITOKEA JIJINI DAR ES SALAAM KUELEKEA NCHINI KONGO NA NDIPO
MSINDIKIZAJI WA MIZIGO YA KAMPUNI YA TRIPPLE “A” YA JIJINI DAR ES
SALAAM ELIA SANGA (22) MKAZI WA D’SALAAM ALIPOGUNDUA KUIBWA KWA VIPANDE
HIVYO NA KUTOA TAARIFA.
BAADA
YA TAARIFA HIZO, MSAKO MKALI ULIENDESHWA NA NDIPO MTUHUMIWA ALIKAMATWA
AKIWA NA KIPANDE KIMOJA CHA SHABA. THAMANI YA MALI ILIYOIBWA BADO
HAIJAFAHAMIKA, UPELELEZI UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA KUKITAFUTA
KIPANDE KINGINE AMBACHO BADO KUPATIKANA.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R.
WANKYO ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA KATIKA MAMLAKA HUSIKA
ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI LA WIZI ILI WAKAMATWE. AIDHA
ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA
WANAOWAKAMATA WA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI
ZA KISHERIA.
Imesainiwa na:
[NYIGESA R. WANKYO – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment