Moja kati ya kitendawili kigumu kwa vyama vya siasa nchini ni iwapo watakubali matokeo kama watashindwa katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu, swali hilo limekutana na majibu ya CCM.
Akijibu
swali hilo jana alipozungumza na waandishi wa habari, mjumbe wa kamati
ya kampeni ya CCM, January Makamba alisema kuwa chama hicho hakina wazo
la kushindwa kwa kuwa uwezekano huo haupo.
“Tangu
mwanzo, uwezekano wa kushindwa haujakuwapo na hatujawahi kufikiria
kwamba tutashindwa kwa sababu hilo halipo akilini kutokana na idadi ya
wanachama wa CCM na ubora wa Dkt. Magufuli,” alisema January.
Mwishoni
mwa mwezi Septemba mwaka huu, mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa
aliulizwa swali hilo wakati akiongea na kituo cha runinga cha Citizen
cha nchini Kenya.
“Siwezi kusema nitachukulia kama nimeshindwa hadi nitakapothibitishiwa kuwa kila kitu kimeenda sawa kama hakuna hujuma,” alisema Lowassa na kuongeza.
“Tunaogopa sana kuhusu hujuma, kila mtu unaeongea nae unapokutana nae anakwambia ‘utashinda, lakini je, watakubali kushindwa?”
“Tunaogopa sana kuhusu hujuma, kila mtu unaeongea nae unapokutana nae anakwambia ‘utashinda, lakini je, watakubali kushindwa?”
Post a Comment