Shirika
la umeme nchini Tanesco limesimamisha uzalishaji wa umeme katika Bwawa
la Mtera baada ya mitambo yake kuzimwa katika kipindi cha wiki moja sasa
kutokana na kupungua kwa kina cha maji katika Bwawa hilo linalozalisha
megawati 80 ambacho ndicho kiwango cha juu kabisa kuzalishwa na Bwawa
moja hapa nchini.
Meneja
wa Tanesco kituo cha kuzalisha umeme cha Mtera mhandisi Abdallah Ikwasa
amewaambia waandishi wa habari waliotembelea kituo hicho kujionea hali
halisi ya uzalishaji umeme kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na
kupungua kwa kina cha maji katika Bwawa hilo hata baada ya kituo hicho
kulazimika kuzalisha umeme chini ya mita za ujazo zinazoruhusiwa
kitaalam.
Aidha
muhandisi Ikwasa amesema kufuatia hali hiyo Kwasasa Tegemeo pekee la
nishati ya umeme ni mitambo ya kuzalisha umeme inayotumia gesi asilia
ambayo shirika bado linaendelea na hatua za uimarishaji vituo vyake kwa
lengo la kuondoa adha ya kukatika kwa umeme katika maeneo
yaliyounganishwa kwenye gridi ya taifa.
Post a Comment