JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 09.10.2015.
WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA GARI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
WATU
WAWILI WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA LENYE NAMBA
ZA USAJILI T. 440 AXX AINA YA MITSUBISHI CANTER IKIENDESHWA NA DEREVA
AITWAYE PWELA MWALEMBO (30) MKAZI WA ILEMBO LILILOKUWA LIKITOKEA KIJIJI
CHA ITUMBA WILAYA YA ILEJE KUELEKEA ITALE ILIACHA NJIA NA KUPINDUKA.
WALIOFARIKI KATIKA AJALI HIYO NI 1. IMANI MBEYALE (27) NA 2. IYELA SAID (33) WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA ITALE.
AJALI
HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 08.10.2015 MAJIRA YA SAA 19:30 USIKU HUKO
KATIKA KIJIJI CHA ISHENTA, KATA YA NDOLA, TARAFA YA BULAMBYA, WILAYA YA
ILEJE, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA ITUMBA/IWIJI.
AIDHA
KATIKA AJALI HIYO WATU 23 WALIJERUHIWA KATI YAO WANAUME 20 NA
WANAWAKE 03 AMBAO WOTE WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA ILEJE.
CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO,
JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R.
WANKYO ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA/ALAMA NA MICHORO YA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
Imesainiwa na:
[NYIGESA R. WANKYO – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment