Na Anitha Jonas- Maelezo
7/10/2015
Dar es salaam
Tume
ya Taifa ya uchaguzi nchini amewaasa wananchi kutosimama katika vituo
vya kupiga kura mara baada ya kupiga kura oktoba 25 mwaka huu kwani
mawakala wa vyama vya siasa wa kuwepo katika vituo vya kupigia kura ili
kulinda maslahi ya chama pamoja na wagombea wao.
Wito
huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian
Lubuva alipokuwa akifungua mkutano wa tume na waratibu wa uchaguzi wa
mikoa, wasimamizi wa uchaguzi na makamanda wa polisi nchini.
Jaji
Lubuva amesema kuwa wajibu wa mawakala ni kuangalia sheria, kanuni na
taratibu zilizowekwa na Tume zinazingatiwa katika mchakato mzima wa
kupiga kura, kuhesabu kura na kutangaza matokeo na pia kulinda maslahi
ya chama au wagombea wao.
“Changamoto
zilizojitokeza katika chaguzi zilizopita ni pamoja na kuwapo na makundi
ya vijana wanaohisiwa kuwa ni wafuasi wa vyama vya siasa kuwatisha
wapiga kura hasa wakinamama ili wasiende kupiga kura”
“Ni
rai yangu kwenu kuhakikisha hilo halijitokezi katika uchaguzi huu kwani
kupiga kura ni haki ya kikatiba ya kila mtanzania hivyo tusiruhusu
vikundi vya watu kuwa karibu na eneo la upigaji kura kwa kisingizio cha
kulinda kura kwani hii itapelekea uvunjifu wa amani” ameongeza Jaji
Lubuva.
Mbali
na hayo Jaji Lubuva amesema lengo la kushirikisha Jeshi la polisi
kwenye uchaguzi mkuu ni kutambua na kuhakikisha kuwepo kwa hali ya
usalama na amani wakati wa uchaguzi kwani uchaguzi huru na wa haki ni
lazima uendeshwe katika hali ya utulivu na amani.
Kwa
uapande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu amesema kuwa
jukumu la jeshi la polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao,
kuimarisha ulinzi katika vipindi vyote na haswa kipindi hiki cha
uchaguzi, kulinda vifaa vya uchaguzi na kusimamia usalama katika vituo
vya kupigia kura.
Post a Comment