Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ujenzi, Segolena
Francis (kulia), akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo asubuhi
wakati akimkaribisha Mkurugenzi wa Barabara wa Wizara ya Ujenzi,
Mhandisi Ven Ndyamkama (kushoto), kuzungumza na waandishi wa habari
kuhusu mafanikio ya serikali katika sekta ya ujenzi kwa kipindi cha
miaka 10 kuanzia mwaka 2005 hadi 2015.
|
Mkurugenzi
wa Barabara wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Ven Ndyamkama (kushoto),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
mchana, kuhusu mafanikio ya serikali katika sekta ya ujenzi kwa kipindi
cha miaka 10 kuanzia mwaka 2005 hadi 2015. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini wa wizara hiyo, Segolena Francis. |
|
Hapa mkutano ukiendelea. Na Dotto Mwaibale
WIZARA
ya Ujenzi imesema itashirikiana na Sekta Binafsi (PPP) kuhakikisha kuwa
baadhi ya miradi ya barabara inajengwa na sekta hiyo ili kukamilisha
miundombinu ya usafiri nchini.
Hayo
yalisemwa na Mkurugenzi wa Barabara katika Wizara hiyo Mhandisi Ven
Ndyamukama wakati akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ukumbi
wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam.
Alisema
mfano wa mradi wa ushirikiano wa Serikali na PPP ni barabara ya Dar es
Salaam hadi Chalinze ambayo itakuwa na njia sita unatarajiwa kuanza hivi
karibuni.
Alisema
lengo la Serikali kushirikiana na sekta binafsi ni kuhakikisha kuwa
miradi mingi inakamilika kwa wakati ambapo kwa kipindi cha miaka 10 ya
Serikali ya awamu ya nne wamekamilisha ujenzi wa kilometa 5,568 za lami
zilizogharimu sh. bilioni 4,090 kati kilometa 17,762 ambazo zilitarajiwa
kujengwa.
"Tumejipanga
kushirikiana na sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi mingi hapa
nchini lakini kwa kuanza ni huu wa Dar es Salaam hadi Chalinze
unaotarajiwa kuanza hivi karibuni," alisema.
Pia
alisema kilometa 3,873 zinaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami kwa
gharama ya jumla ya sh.bilioni 4,533 na barabara zenye urefu wa kilometa
4,965 zimefanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa gharama ya
shilingi bilioni 29.257 ambapo Serikali inatafuta fedha za ujenzi wa
lami.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com
|
on Wednesday, October 7, 2015
Post a Comment