Timu
ya Taifa Tanzania ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars)
inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Wanawake ya
Malawi Novemba 7, 2015 jijini Dar es salaam.
Mchezo
huo wa kirafiki ni sehmu ya kujipima kwa Twiga Stars inayonolewa na
kocha Rogasian Kaijage, ambayo ilishiriki Fainali za Michezo ya Afrika
(All Africa Games) mwezi Agosti – Septemba nchini Congo – Brazzavile.
Awali
Twiga Stars ilikua icheze mchezo huo nchini Malawi Oktoba 24, kabla ya
chama cha soka nchini humo (FAM) kuahirisha mchezo huo, na sasa mchezo
huo utacheza nchini Tanzania Novemba 07, 2015.
Post a Comment