Mkurugenzi wa NEC, Ramadhani Kailima.
Mkurugenzi
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndugu Kailima Ramadhani amefafanua jinsi
mabavyo Tume ya taifa ya uchaguzi ilivyo gawanya vituo vya wapiga kura
kote nchini. Katika ufafanuzi huo amefafanua mambo makuu Mawili.
1.
Namna ambayo siyo sahihi ya kuhesabu vituo vya wapiga KURA kama walivyo
fafamua baadhi ya watu, Ambayo ni namna ya KUPOTOSHA NA NI UWONGO, na
2. Namna SAHIHI ya kuhesabu vituo kama tume ye taifa ya uchaguzi ilivyo hesabu. Nia hii inazingatia mambo yafuatayo.
i). KUTUO HAKITAZIDI WATU 450
ii). KITUO KINAWEZA KUWA NA IDADI CHINI YA WATU 450
ILI WATU WALIOJIANDIKISHA KITUO KIMOJA WASIHAMISHWE KWENDA KUJAZIA ENEO JINGINE.
Itakuwa hivi.
Endapo kuna eneo ambalo watu waliojiandikisha ni 1900 Tume ya taifa ya uchaguzi itagawanya watu kama ifuatavyo:-
450+450+450 = 1300
1900-1300 = 550
550 gawanya kwa 2 = 275
KWA HIYO MAHALI PENYE WAPIGA KURA 1900
PATAKUWA NA VITUO VITANO (5)
1. KITUO CHA KWANZA WATU 450
2. KITUO CHA PILI WATU 450
3. KITUO CHA TATU WATU 450
4. KITUO CHA NNE WATU 275
5. KITUO CHA TANO WATU 275
JUMLA 1900
ZINGATIA
Kutokana na kuwepo kwa vituo vyenye idadi ya watu chini ya 450 kumefanya idadi ya vituo iwe kubwa.
Post a Comment